Wanafunzi wa shule ya sekondari naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara baada ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. |
Press Release
Serikali yaipongeza Airtel kwa kuchangia maendeleo ya elimu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura na kusema kuwa licha ya kuwa ni jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa shule lakini imekuwa ikizidiwa na majukumu mengi hivyo kwa msaada huo Airtel wanapaswa kupongezwa kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa msaada wa vitabu kwa Shule ya sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya mpango wake maalumu wa “shule yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela alikuwa mgeni rasmi.
Bwana Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo ya msingi ya kupata maarifa hivyo kwa Airtel kujikita katika kusaidia jamii kupitia vitabu kwa shule za sekondari kutawawezesha wanafunzi na jamii kupata hazina kubwa ya maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia vitabu hivi. Napongeza sana jitihada hizi na mpango huu ambao ni endelevu na yenye kugusa shule nyingi na jamii kubwa ya watanzania kwa ujumla”.
Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala akizungumzia msaada huo amesema mpango huo unaolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni yaani vitabu vya hisabati, physikia, chemia na biologia una lengo la kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni, tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari Naura kwani tunaamini wanafunzi wengi zaidi watanufaika na kuhamasika kujiunga na kusoma masomo ya sayansi
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Gasper Mushobozi aliwashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu vya sayansi shuleni hapa , lakini alibainisha kuwa msaada huu pia uendelezwe kwa kutuboreshea maabara ya shuleni hapo ili kuweza kupata tecknologia ya sayansi kikamilifu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.