ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 2, 2019

Wananchi watakiwa kujitokeza kuchangia damu kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani



Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wanachi ndani ya Mkoa huo kuwa tayari kujitokeza katika Zoezi la Uchangiaji wa damu Salama linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

RC Ayoub alisema Zoezi hilo lina lengo la kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji Damu kutokana na maradhi mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga Mjini Magharib Unguja Ayoub alisema imekuwa utaratibu ambao umezoeleka kila ifikapo karibia na mwezi mtukufu wa Ramadhan  wananchi ndani ya Mkoa huo kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa vifo vitokanavyo na mahitaji ya Damu.

Pia aliongeza kuwa ukusanyaji wa damu salama una lengo la kuwasaidia wananchi katika kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu wa mfungo wa ramadhani hasa kwa akina mama wanaojifungua na watoto ambao asilimia kubwa ndio wanaohitaji damu hiyo.

Alieleza kuwa katika kipindi cha mfungo huo wa ramadhani mara nyingi si vyema watu kuchangia damu kutokana na hali ya kiafya ambapo katika kipindi hicho cha mwezi mzima kumekuwa na mahitaji makubwa kwa kitengo cha damu salama ambapo kinahitaji ujazo wa unit 1700.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa alisema kitengo hicho cha damu salama kimesha kusanya unit 1400 katika kipindi hichi kwa ajili ya kuelekea mfungo wa ramadhani na kwamba wameshatumia unit 400 kwa muda wiki mbili zilizopita hivyo bado kunahitajika kuchangia damu hiyo ili kufikia malengo hayo.

Zoezi hilo la Uchangiaji wa Damu Salama linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.