ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 21, 2011

DIWANI STANISLAUS MABULA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE.

DIWANI wa Kata ya Mkolani ameanza utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi zake kwa kutoa msaada wa mifuko 45 ya Saruji na kuchangia Shilingi 350,000/- za gharama ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi katika Sekondari ya Luchelele na shule ya msingi Mkolani Wilayani Nyamagana.Akikabidhi mifuko 25 ya saruji kwa Uongozi wa shule ya msingi Mkolani jana Diwani Stanislaus Mabula wa Kata hiyo(CCM),amesema kwamba tangu kumalizika kwa uchaguzi ameanza kutembelea Kata yake kufatilia kero ambazo ameanza kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo ya kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita.

Diwani Stanislaus Mabula (aliyenyoosha kidole) akipata maelezo ya mipaka ya eneo la chumba cha darasa na ofisi mpya za walimu toka kwa mkuu wa shule mwalimu Mbokela Sahani (mwenye shati-njano), mbele ya mtendaji wa kata Mtani Evarist (mwenye shati-pinki) na anayeandika ni afisa maendeleo kata Raphael mphulu.

Huku wengine wakijisomea ni Wakati wa mapumziko wanafunzi ndani ya moja ya madarasa ya shule hiyo.

Mheshimiwa akishiriki kuondoa nyasi zilizoota eneo la shule.

Hili ni Darasa kamili na madawati yake.

UHABA WA VYOO.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo ambaye ni Msaidizi mwalimu Mbokela Sahani akipokea msaada huo wa Saruji amesema kwamba viongozi waliopo kwenye Kata hiyo kwa kushirikiana na wazazi waendelee kuisaidia shule hiyo kwakuwa bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa madarasa, Ofisi za walimu (Staff), maktaba na matundu ya vyoo ambayo hayatoshi na yamekwisha jaa.

Wataalam wetu wa kesho katika kamera yako.

PICHA YA PAMOJA.
Mabula amewataka walimu hao kutokubali kutumiwa na baadhi ya watu na wanasiasa kwa lengo la kudhoofisha utoaji wa taaluma na badala yake matatizo yao yapelekwe kwenye vyombo husika ili serikali iyatafutie ufumbuzi wa haraka huku wao wakihakikisha elimu na ufaulishaji wanafunzi katika shule zao ukiboreka kila mwaka na maadili ya watoto yakiwa mazuri.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Hi! gsengo
    hongera sana na unajitahidi kuwaelimisha,kuwaburudisha na kuwahabarisha watu wa kanda ya ziwa na maeneo ya jirani kwa blog yetu hii kanda ya ziwa.
    mimi
    Peter kaseko
    tuko pamoja

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.