ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 20, 2011

MWANZA BEST OFFICERS AWARDS

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Saidi Mwema kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, wametoa jumla ya shilingi milioni 3200000/= kwa askari 31 walioshiriki katika tukio la kupambana na majambazi lililotokea desemba 29 mwaka jana katika kijiji cha kanyama wilaya ya Magu mkoani hapa.Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akikabidhi cheti na pesa taslimu kwa mmoja wa polisi walioshiriki zoezi la kupambana na majambazi wezi wa magari, mapambano yaliyotokea katika Kijiji cha Kanyama, Kata ya Kisesa wilayani Magu, mkoani Mwanza.

Sherehe fupi ya kuwapongeza Askari hao iliyokwenda sanjari na kuwakabidhi fedha na kuwatunuku vyeti imefanyika leo asubuhi katika uwanja wa polisi mabatini jijini Mwanza na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za wilaya na mkoa.

"Jeshi la polisi ngazi ya mkoa tulipanga kutoa kiasi hicho cha fedha nilichokitaja lakini mkuu wetu wa kazi IGP Mwema kwa kutambua kazi nzuri waliyo ifanya vijana hawa akaongeza sh, 50,000/= kwa kila mmoja, vivyo leo tutawakabidhi shilingi lakimoja kila mmoja na kwa wale majeruhi wawili watakabidhiwa shilingi lakimoja na elfu hamsini kila mmoja" Kaimu kamanda wa pilisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba Akiongea wakati wa kumkaribisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kamanda Komba amesema hali za majeruhi wote wawili zinaendelea vizuri ambapo PC Erasto aliyejeruhiwa kwa risasi katika paja na mkono wake wa kulia ameruhusiwa kutoka hospitalini wakati CPL jumanne aliyepigwa risasi mbili begani katika mkono wake wa kushoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando
Gwaride la jeshi la polisi.

Wakati mgeni rasmi akihutubia, askari huyu aliyekuwa yummoja kati ya waliokuwa wamesimama wima ktk rigwaride wakisikiliza hotuba alianguka ghafla, Pichani akipelekwa eneo la huduma ya kwanza.

Aidha mkuu wa mkoa wa Mwanza amewataka wananchi kuheshimu utawala wa sheria kwa vile nchi inaongozwa kwa misingi ya kanuni na taratibu za utawala bora, wananchi waachane na dhana mbaya ya kuchukuwa sheria mkononi bali wanapomtuhumu au kumkamata mhalifu ni vyema wakamkabidhi mikononi mwa polisi ili sheria zichukuwe mkondo wake.

Picha ya pamoja askari waliotunukiwa na kaimu kamanda wa polisi.

Picha ya pamoja viongozi wa serikali pamoja na askari waliotunukiwa.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. wametunukiwa kwa uhalifu wkt wa uchaguzi mkuu, huyo afande aliyeanguka kaka ni hali ngumu ya maisha tumboni hamna kitu

    ReplyDelete
  2. Kama kwenye gwalide wanadondoka rwanda na malawi wataziweza?

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.