ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 26, 2022

SERIKALI YATANGAZA VIJIJI VITANO, VITONGOJI 41 KUONDOLEWA HIFADHI YA USANGU

GY3A7799 Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta wanaoushughulikia migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisoma majina ya vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya Mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.



SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi imetangaza kwamba vijiji vitano na vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha Magwalisi ambacho kipo kwenye Mamlaka ya Mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali wananchi wanatakiwa kuhamishwa ili kupisha hifadhi.


Akitangaza uamuzi huo leo Oktoba 25 mwaka 2022 ,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula amesema katika uamuzi huo pia vitongoji vitatu katika kijiji cha Lualaje wilayani Chunya navyo vinatakiwa kuondoka kupisha hifadhi.

Akieleza zaidi mbele ya wananchi wa Ubaruku wilayani Mbarali wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta walipofanya ziara kwenye eneo la Mto Ruaha Mkuu ,Dk.Mabula amesema lengo la uamuzi ni kutunza na kulinda ardhi oevu na vyanzo vya kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali.

Dk.Mabula amevitaja vijiji vitakavyoondoka kwa asilimia 100 ni Madundasi, Luhanga, Iyala, Msanga pamoja na Kalambo yo vina idadi ya wakazi 21,252 na kusisitiza watu wa maeneo hayo wanatakiwa wasiwepo na usajili wa vijiji hivyo kufutwa.

Ameongeza kwamba kwenye mchakato huo wapo ambao watalipwa fidia na wengine ambao hawastahili Kulipwa fidia wataondoka kama walivyokwenda huku akisisitiza lengo la Serikali ni kuwa na urithi wa watu wote."Mnakumbuka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuja na kuahidi kushughulikia migogoro ya ardhi ,Sasa tumekuka na uamuzi ambao tutaomba."

Pamoja na hayo amesema pia Serikali imeridhia vijiji 15 ambavyo vina ukubwa wa hekta 74, 324.12 na ranchi ya Usangu ya NARCO vitaendelea kubaki wakati vijiji vingine vyote vinavyopakana na hifadhi ya Ruaha kutawekwa mipango mikakati ya mpango wa matumizi ya ardhi.

"Kwenye mapendekezo ya timu ya wataalamu ilipendekeza Ranchi ya Usangu ambalo linalopendekezwa kuondolewa ndani ya hifadhi litumiwe na wafugaji watakaohamishwa kutoka kwenye vijiji na vitongoji vinavyopisha hifadhi, " amesema Dk.Mabula.

Pia ameeleza Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya za Mbarali na Chunya pamoja na wadau wanatakiwa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vyote vinavyopatikana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Kwa mujibu wa Dk.Mabula TAMISEMI inatakiwa kushirikiana na wadau muhimu wakati wa mchakato wa usajili wa vijiji na vitongoji kwa ajili ya kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza na kusababisha malumbano yasiyo na tija.

Kuhusu bonde la Uhifadhi wa Bonde la Usangu imeelezwa kwamba ulianza mwaka 1953 na wakati huo kama pori tengefu la Utengule lenye ukubwa wa kilomita za mraba 500 kwa lengo la kuhifadhi bioanuwai katika ardhi oevu ya Ihefu.

kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira na vyanzo vya maji uliofanyika miaka ya 1990 serikali iliamua kupandisha hadhi pori tengefu la utengule na kuwa Pori la Akiba la Usangu likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4148 kwa tangazo la serikali namba 436A la tarehe 24 julai 1998.

Pamoja na hayo amesema Serikali imekuja na mpango wa kitaifa wa hifadhi ya mazingira ya ardhi oevu na vyanzo vya maji mwaka 2006 na kutaka bonde la Usangu kuwa kati ya maeneo ambayo wafugaji waliovamia mabonde na maeneo ya vyanzo vya maji waondolewe.

GY3A7807Baadi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ubaruku,Mbarali mkoni Mbeya leo Oktoba 24,2022.
GY3A7816Baadi ya Wananchi wakiondokoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ubaruku,Mbarali mkoni Mbeya leo Oktoba 24,2022 ambapo Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wa Wizara nane za Kisekta wanaoushughulikia migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisoma majina ya vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya Mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.
GY3A7467
Timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiongozwa na Mwenyekiti wao Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Homela walipokwenda kutazama na kujionea hali halisi ya upungufu mkubwa wa maji katika mto Ruaha Mkuu leo Oktoba 24,2022,Mbarali mkoani Mbeya. 
GY3A7471
Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja,kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.

PICHA ZOTE NA MICHUZI JR.MBARALI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.