ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 25, 2022

RC DR ES SALAAM ATANGAZA HALI YA UKAME KATIKA MTO RUVU.


Na Victor Masangu,Pwani 

Serikali imesema kwamba kwa sasa hali ya kiwango cha uzalishaji wa  maji katika mto Ruvu  kimepungua kwa asilimia 64  kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa  ukosefu wa mvua za vuli uliosabishwa na madaliko ya tabia ya nchi na kupelekea kuwepo kwa ukame.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa Dawasa , pamoja Kamati ya ulinzi na usalama ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea hali halisi ya kupungua kwa kiwango cha maji.
 
Aidha mkuu  huyo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Pwani na Morogoro amesema kwamba jitihada za serikali katika kuhakikisha maji yaliyopo yanawafikia wananchi japo kwa mgao hadi hapo mvua zitakaponyesha.

Makala alisema kwamba hali hiyo ya kupungua kwa kiwango maji katika mto ruvu kumesababishwa na kukosekana kwa mvua za vuli hivyo kwa sasa kutalazimika kuwa na mgao katika maeneo mbali mbali.

"Tumejionea kushuka kwa kina na uzalishaji katika mitambo ya ruvu juu pamoja na ruvu chini na kwa hali hii ni lazima tuchukue tahadhari na wananchi wahakikishe kwamba wanatunza maji kwani yatakuwa ya mgao,"alisema Makala.

Pia  Mkuu huyo ya Mkoa alibainisha kuwa kasi ya  uwezo wa uzalishaji wa maji umeshuka kutoka  Lita Milioni 466 mpaka kufikia lita zipatazo  Milioni 300 hivyo kiwango cha maji kimeoungua.

"Ndugu zangu wananchi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Dar es Salaam kumuomba Mungu ili mvua  ziweze kunyesha  na kutumia vizuri kiasi cha maji yaliyopo ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji huo wa maji,"alibainisha Makala

Mkuu huyo wa Mkoa alisema  tatizo la mgao wa maji katika jijini la Dar es Salaam  kwa Sasa ni matokeo ya kiangazi kilichosababishwa na kukosekana kwa mvua za vuli  jambo lililopelekea kushuka kwa kina Cha maji kwenye vyanzo vya Maji Ruvu juu na ruvu chini.

Aidha aliongeza Kamati za Ulinzi na usalama Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro zilishatekeleza wajibu katika   kudhibiti uchepushaji wa maji hivyo uhaba wa maji hauhusiani na uzembe wa mamlaka husika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.