ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 13, 2013

BALOZI WA CHINA NCHINI AAHIDI KUSAIDIA KILIMO CHA MAHINDI SONGEA


Mwenyekiti wa CCM Oddo Mwisho akimpa zawadi ya kinyago balozi wa China anaye shuhudia kulia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Joseph Mkirikiti. 

   
 Mwenyekiti wa Halmashauli ya Songea vijijini Rajabu Mtiula akimpa Kapu  Balozi wa China,Katikati Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama. 
 

Mzee wa kimilila amabaye jina lake halikufahamika mara moja akimvesha mgorori balozi wa China Nchini Tanzania Lu Younqing. 
 
Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Revocatus Kasimba akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga Kulia.
    
............................................................................................................................

BALOZI wa china nchini Tanzania Lu Younqing ambaye yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku tatu ameahidi kuleta wawekezaji zaidi na watalaamu wengi katika sekta ya kilimo cha mahindi ili kulifanya zao hilo liwe  la kibiashara linalozalishwa kwa njia ya kilimo cha kisasa zaidi na kuwafanya wakulima wa zao hilo kujikwamua zaidi kichumi   .
 
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa siku ya kwanza ya   ziara yake alipokuwa akikagua mashamba mbalimbali ya kilimo cha mahindi ambacho kinachofanywa na wakulima wa zao hilo latika jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma .
 
Katika ziara hiyo ya balozi Lu Younqing alitoa misaada mbalimbali kwenye vikundi vya kijamii na wakulima vilivyopo katika jimbo la Peramiho ikiwemo shule ya sekondari ya Namihoro iliyopo katika kijiji cha peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.
 
Vikundi hivyo vilivyopata msaada huo ikiwemo  sekondari ya Namihoro iliyopewa shilingi milioni 10 ili kuendeleza elimu katika shule hiyo ,kikundi cha wakina mama wajasiriamali kilipewa  vyerehani 20 ili wajikwamue kiuchumi na baiskeli 20 kwa viongozi wa jumuiya ya vijana wa CCM wa kata zote za jimbo hilo la Peramiho.
 
 Aidha balozi huyo kabla ya kuhitimisha ziara yake hiyo ya siku tatu atatembelea pia mashamba ya kilimo cha kahawa yaliyopo katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ili kubaini changamoto zinazokabili kilimo hicho na kuwa akielekea wilaya ya Mbinga amepita kwenye barabara ya kiwango cha lami iliojegwa na nchi ya China kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.
 
 Ziara hiyo ya balozi wa China kutembelea mkoa wa Ruvuma umekuwa ni mwaliko rasmi wa mbunge wa jimbo la Peramiho kwa tiketi ya chama cha mapinduzi  Jenista Mhagama ambaye aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutumia fursa hiyo ya ujio wa balozi huyo kwa kufanya kazi zaidi katika kilimo kwa sababu balozi huyo ameahidi kulifanya zao la mahindi kuwa zao la kibiashara.
 
 Alisema kuwa kilimo cha kisasa ndicho kinachoweza kuwakwamua zaidi kuichumi na kuondokana na wimbi la umasikini linalowakabili pia aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo na misaada iliyotolewa kwao na balozi huyo kama changamoto kwao katika kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini uliopo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.