ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 14, 2019

WAZIRI UMMY AKANUSHA KUWEPO MGONJWA WA EBOLA NCHINI.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, ametoa tahadhari na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ili ugonjwa wa Ebola usiingie hapa nchini.

Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo wakati akitoa taarifa za uvumi wa uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini na kuwatoa hofu wananchi kuwa hakuna dalili za ugonjwa huo kuwepo licha ya kuripotiwa katika nchi jirani.

''Naomba niwatoe hofu wananchi, hadi sasa hakuna mgonjwa yoyote wa Ebola aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo'', amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amezitaja dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni homa kali, kuumwa kichwa, kutapika na kuharisha, viungo vya mwili kuuma pamoja na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili.

Waziri Ummy ameongeza kuwa licha ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupeana mikono ni vyema ukawekewa tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.