ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 9, 2019

PSS FORUM YAWEKA MIKAKATI YA ULINZI KWA WATOTO AFRIKA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REPPSI Lynette Mudekunye na Mwenyekiti wa Bodi ya REPPSI Tanzania wakiwa kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia. 

Mkurugenzi Mkazi wa REPPSI Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia
 wadau na viongozi wakiwa kwenye kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia

 Tumaini Godwin, Namibia

 Nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zinaweza kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia.

Profesa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Hosea Rwegoshola amesema hayo wakati akiwasilisha utafiti wake kuhusu kuimarisha malezi mbadala ya watoto, katika mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto (PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.

Profesa Rwegoshola amesema kupitia utafiti alioufanyia katika kata ya Chanika jijini Dar es Salaam, watoto wanaweza kuwa salama ikiwa ulinzi wao utaanza kuimarishwa kuanzia ngazi ya familia.

"Kwa hiyo matokeo ya utafiti wangu ni kwamba familia mbadala zinaweza kusaidia malezi ya watoto, na hizi zikiimarishwa tatizo la watoto mitaani linaweza kupungua, ukatili majumbani utakoma," amesema.

Ametaja familia mbadala kuwa ni pamoja na ndugu wa ukoo kulea watoto, walezi wakujitolewa na wale wanaorithi watoto kisheria.

Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF)nchini Namibia Rachel Odede amesema mazingira bora ya mtoto kukua ni kwenye familia.

"Mamilioni ya watoto wameachwa nyuma kwenye malezi na takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watano analelewa bila familia, mtoto anatakuwa kukua kwa furaha," amesema Odede.

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) Tanzania Edwick Mapalala amesema ulinzi wa mtoto unapaswa kuanzia ngazi ya familia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.