ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 10, 2019

WAJUMBE WA CCM GANGILONGA WACHANGIA DAMU NA MISAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA IRINGA.

  Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa katika zoezi la kuchangia damu katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia damu
  Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa na wadau wa chama cha mapinduzi wakienda kuwajulia hali wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwapa zaidi mbalimbali
Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa kwenye picha ya pamojana wadau wa kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRNGA.

WAJUMBE wa chama cha mapinduzi kata ya Gangilonga wamejitokeza kwa kujitolea kuchangia damu na kutoa msaada kwa wagonjwa wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa lengo la kuadhimisha Gangilonga ya kijani

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo leonard Raphael Mgina alisema kuwa katika kuadhimisha Gangilonga ya kijani kwa kujitolea damu na kuwaona wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo hapa nchini.

“Tumepita kwenye hodi kumi na tatu kuwaona wagonjwa pamoja kufanya zoezi la kujitolea damu kwa lengo la kusaidia kupunguza upungufu wa damu kwa maana mara kwa mara tumesikia hata kwenye vyombo vya habari kuwa kuna upungufu kwenye benki ya damu” alisema Mgina

Mgina alitoa rai kwa wananchi wengine kuendelea kuchangia damu kwa kuwa hakuna aijua kesho yake hivyoni muhimu kuwa na moyo wa kujitolea kutoa damu ili kupunguza upungufu wa damu uliopo katika benki za damu katika hospitali zetu zote hapa nchini.

Naye katibu wa chama cha mapinduzi kata ya hiyo Likotiko Kenyatta alisemalengo ni kuhakikisha wajumbe na wadau wa chama cha mapinduzi nikurudisha fadhila kwa jamii kama ambavyo wamefanya katika siku ya Gangilonga ya kijani.

“Leo tumekuja kufanya shughuli za kijamii, kugawa misaada pamoja nakutoa damu kwa lengo la lakukihusisha chama cha mapinduzi katika shughuli zote za kijamii na kuifanya kata ya Gangilonga kuonekana ya kijani kweli kweli” alisema Kenyatta

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa chama cha mapinduzi wa kata hiyo wamempongeza diwani wa kata hiyo kwa kuendelea kuing’alisha Gangilonga ya kijani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.