Mtihanin wa Darasa la Saba umepangwa kufanyika kwa kipindi cha siku mbili Septemba 11 na 12 mwaka huu kote nchini ambapo hii leo Katibu Mkuu CWT,Mwalimu Seif amezungumza na waandishi wa habari na kuwaomba waalimu kuwa waaminifu katika kipindi chote cha Mitihani.
"Tunajua moja ya kazi kubwa ya Chama cha waalimu ni utetezi,na moja ya sehemu ya utetezi ni matatizo ya ufujaji wa mitihani ambao kimsingi wasimamizi ni walimu,sasa mimi naomba niwaambie walimu wangu kuwa kazi ya kufundisha wameimaliza wiki iliyopita,sasa hivi waache watoto wafanye mitihani,nawaomba wawe waaminifu kwenye zoezi la kusimamia mitihani"Alisema.
Aidha kufuatia baadhi ya shule za binafsi kuhusishwa katika tuhuma za kuiba mitihani Mwalimu seif ametoa wito kwa Viongozi na waalimu wa shule hizo
"Pamoja na kuwa tuna idadi ndogo ya wanachama kutoka shule za Private,niwaase tu wawe waaminifu kwani kama wakiendelea kutuhumiwa watashusha hadhi yao kwa wateja wao"Alisema.
Mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Chemba ilifutiwa matokeo ya mtihani wa Darasa la saba kwa makosa ya kufanya udanganyifu,kwa mwaka huu Kituo hiki kimezungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Semistatus Mashimba ambaye yeye amesema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga vyema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.