ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 10, 2019

TANZANIA YAWEKEZEA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WATOTO NA WANAWAKE

 Dr Naftari Ng'ondi kamishina wa ustawi wa jamii nchini Tanzania  amesema serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia

Tumaini Godwin,Namibia.

 Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Dk Naftari Ng'ondi amesema hayo  wakati akiwasilisha mkakati huo kwenye mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto(PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.

Dk Ng'ondi amesema mkakati huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2016  umetamka wazi kuwa pamoja na mambo yote, tatizo la mimba na ndoa za utotoni linapaswa kushughulikiwa.

"Mimba za utotoni maana yake kuna ubakaji umefanyika na  kwa Tanzania hilo ni kosa la jinai, tumeimarisha sheria ya mtoto na yeyote anayekutwa na kosa la kumpa mimba mwanafunzi anafungwa jela miaka 30," amesema Kamishna huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Amesema mbali na sheria, wanatekeleza mkakati huo kwa kuikarisha kamati za ulinzi wa mtoto kwenye kata kwa kuzipatia nguvu ya kupokea, kuchunguza na kuchukua ikiwa ni pamoja na kufungua kesi.

Dk Ng'ondi amesema nguvu kubwa imewekwa katika kutoka  elimu kwa Jamii na vijana kupitia kampeni mbalimbali.

"Na sasa hivi tunaendesha kampeni inayoitwa Twende pamoja, tokomeza ukatili," amesema.

Awali Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Mpango wa kutokomeza mimba za utotoni, Nyaradzayi Gumbonzvanda alisema nchi za Afrika zinapaswa kufanya kampeni ya kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni linaisha.

Amesema nchi nyingi za Afrika zinakutana na changamoto ya mimba za utotoni huku umaskini ukichangia tatizo hilo.

"Tuandae mkakati ya kumalizaa tatizo,inawezekana," amesema Gumbonzvanda.

Mkutano huo unaoendeshwa na Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) umezikutanisha zaidi ya nchi 24 kutoka kusini mwa Afrika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.