Shoot ....ya ufunguzi. |
Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya george Mbijimana akipigiwa makofi mara baada ya kufungua rasmi mashindano. |
Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya
mchezo wa Pool Taifa zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia
yake ya Safari Lager zimeanza rasmi jana Mkoani mbeya zikishilikisha vilabu
tisa vya mkoani humo.
Akifungua fainali hizo
Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima aliwaomba wachezaji kuwa na
watulivu na kuzingatia nidhamu ya mchezo ili mwisho wa fainali apatikane
mshindi atakaebeba bendera ya Mkoa wa mbeya kwenye fainali za kitaifa na arudi
na ushindi.
Mbijima alisema taswila
ya mchezo wa Pool si nzuri sana miongoni mwa watu kwani unatazamwa kama mchezo
wa wahuni na hakuna mtu mwingine wa kubalilisha zaidi ya wachezaji wenyewe, hivyo
kuweni na nidhamu ili hata jamii ifike mahala itambue kumbe pool ni mchezo kama
michezo mingine.
Mbijima pia aliishukuru
TBL, kupitia bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani
kwa kufanya hivyo inawafanya vijana kuepuka vitu vingi ikiwemo uhalifu,kukaa
vijiweni bila kazi lakini sasa wananufaika chochote kutokana na
zawadi wanazopata ukizingaatia michezo ni ajira,michezo burudabi na michezo ni
kufahamiana.
Nae Meneja matukio wa
TBL Mbeya,Godfrey Mwangugulu aliwatakia wachezaji michezo mema na yenye amani
mwisho apatikane bingwa wa haki atakaye wakilisha vyema Mkoa wa Mbeya
Mwisho Mwenyekiti
alivitaja vilabu vinavyoshiriki fainali za Safari Pool Mkoa wa Mbeya kuwa ni
Tunduma Kontena Klabu,Royal Zambezi Klabu,Royal Glass Klabu,Shooters
klabu,Luanch time klabu,Mbeya snukers klabu,Kizota klabu,Makonde klabu na
Terminal Stand klabu.
Zawadi katika
fainali hizo upande wa timu,bingwa atajnyakulia fedha taslimu shilingi
700,000/=,mshingi wa pili 350,000/=,wa tatu 200,000/= na wanne 100,000/ na timu
nane zitakazoingia robo fainali zitapata kifuta jasho cha fedha taslimu
shilingi 50,000/= kila moja.
Upande wa mchezaji mmoja
mmoja(Singles), wanaume bingwa atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi
350,000/=,wa pili 250,000/=,wa tatu 150,000/= na wanne 100,000/= na upande wa
kinadada bingwa atajinyakulia fedha taslimu shilingi 250,000/=,wa pili
150,000/=,wa tatu 100,000/= na wanne 50,000/=.
Fainali za mashindano
hayo zinatarajiwa kumailizika mwishoni mwa wiki hii ambapo mgeni rasmi atakayefunga
anatarajiwa kuwa RPC wa mkoa huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.