Meneja wa Kituo cha Sayansi cha Sterm Park Max George akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani
KITUO cha Sayansi cha Sterm Park cha Jijini Tanga kimetumia wiki ya Sayansi Afrika kutoa mafunzo ya Hisabati ,Teknolojia na uhandisi kwa wanafunzi 350 wa shule mbalimbali za msingi zilizopo jijini hapa yakilenga kuongeza ari kwa wanafunzi kupenda kujifunza masomo ya sayansi kwa malengo yao ya baadaye na kuja kulisaidia Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Sterm Park Max George amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho kimeweza kusaidia na kuongeza ari kwa wanafunzi wengi kupenda kujifunza masomo ya sayansi na hisabati hatua ambayo inaleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla juu ya kile kinachoelezwa kuwa masomo hayo ni magumu.
Alisema kuwa wanafunzi hao wa shule za msingi ambao wamejitokeza na kupata bahati ya kujifunza technologia, uhandisi pamoja na hisabati ni mwanzo wa Juni 26 hadi 30 mwaka huu ambapo kutakuwa na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa mbalimbali ambao watajifunza teknologia ya juu kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikipelekea na adha mbalimbali.
“Tumesherehekea wiki ya sayansi kwa Afrika na watoto 350 kutoka shule mbalimbali za msingi wanaopatikana hapa jijini Tanga wamejifunza juu ya maswala ya hisabati , uhandisi na techolojia kwa vitendo na katika mwendelezo wa kuhakikisha vijana wanedelea kujifunza kwa vitendo zaidi tarehe 26 hadi 30 tutakuwa na vijana wa sekondari kutoka mikoa tofauti toafauti ya Tanzanzia na wao watatengeneza projekti ambayo itakwenda kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.” Alisema Max.
Awali akizungumza Dkt. Isaya Ipiana ambaye ni balozi wa Next Einstein Forum ambao ni waandaaji wa makongamano ya sayansi Afrika kwa wakishirikiana na Sperm Parka katika mkoa wa Tanga amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika sekta ya elimu ikiwemo miundombinu na mabadiliko ya sera ambapo ameiomba serikali kuzidi kuboresha sekta hiyo kwa kuongeza vifaa vya kujifunza na kujifunzi ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuelewa zaidi.
Aidha alisema wanaipongeza serikali kwa kuwa imekuwa ikifanya mabadiliko katika sera mbalimbali za elimu lakini imekuwa inaruhusu wadau wanohusika na masuala ya elimu kufanya kazi katika mazingira mazuri hivyo wao kama wadau wataendelea kuhakikisha wanasonga mbele
Kituo hicho cha Sterm Park kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga june 23 imeandaa tuzo maalum ambazo watatrunukiwa walimu wa kike wanaofanya vizuri katika masomo ya hesabu pamoja na sayansi hii ikilenga hasa kuongeza hamasa kwa walimu kuongeza molari ya kufanya kazi na wanafunzi kupenda na kuwa mabalozi kwa wengine juu ya masomo ya sayansi na hisabati .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.