
Madai hayo yalitolewa jana na Meya wa Jiji, Josephat Manyerere (Chadema), wakati akizungumza wa waandishi wa habari ambapo alidai kwamba ofisi yake haikupewa taarifa ya operesheni ya kuondoa wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara katika mtaa wa Makoroboi.
Alipofuatilia, alibaini kuwa hata ofisi ya Mbunge wa Nyamagana, haikuwa na taarifa ya operesheni hiyo, ambayo imesababisha watu saba kujeruhiwa na kwamba habari zilizoenezwa kuwa Chadema walihusika na vurugu hizo kwa sababu halmashauri
inayoongozwa na chama hicho ni ya uchochezi.
Aidha, ametoa wito kwa wamachinga kujitahidi kupanga bidhaa zao vizuri, ili watu wapate njia ya kupita na pia wasitumie vipaza sauti kutangaza bidhaa zao na kuhakikisha maeneo ya biashara yanabaki safi na wafanye biashara hizo kuanzia saa 10 jioni.
Amewaomba wenye misikiti na shule katika mtaa wa Makoroboi waendelee kuwavumilia hadi ufumbuzi wa kudumu utakapopatikana kutokana na kwamba kulegalega kwa uhusiano wa kikazi kumesababisha vurugu zilizotokea juzi.

Sirro amesema hali jijini hapa ni shwari na majeruhi watatu wameonekana kuwa na majeraha ya risasi za Shot gun na uchunguzi unafanywa kubaini walipigwa na nani kama ni mgambo au kwenye maduka waliyovamia.
Wenje amesema kuwa yuko tayari kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) The Hague, Uholanzi katika suala la kutetea haki za wamachinga kufanya biashara katikati ya Jiji.
Hata hivyo, Mbunge huyo amemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kuchunguza chanzo cha mgambo kupiga watu risasi kutokana na majeruhi wengi wa vurugu hizo kuwa na majeraha ya risasi za bunduki ambazo hazimilikiwi na Polisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.