ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 6, 2011

VURUGU ZA MACHINGA ZASABABISHA MAUAJI MWANZA RISASI ZARINDIMA WATANZANIA WENYE ASILI YA ASIA WAPATA MISUKOSUKO

Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.Kamanda Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.

Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.

Friji ikiteketea..
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.

Kusanyiko la shaka-shaka.

Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..

Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.

Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.

Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.

Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.

Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.

Kuvunjwa vioo kwa jengo hili la msikiti wa hindu ni moja kati ya hasara zilizojitokeza.

Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.

Tupe maoni yako

7 comments:

  1. Duh! kaka G hii ina matrooooooooooo, isee watu wana hasira sana. Pole zetu wakazi wa mwanza.

    ReplyDelete
  2. Duh! Indians should leave our country and businesses. They should go back to their war in pakistan!

    ReplyDelete
  3. anonymous hapo juu inaonekana una chuki binafsi!kuna watanzania wenye asil ya kihindi ,kisukuma kichaga kijaluo na makabila mengi
    mimi noana wewe unamatatizo ya ubaguzi wa rangi na kidini kwani unaongelea wahindi waende pakistani hayo ni mataifa mawili tofauti,na mimi kama mkazi wa mwanza hakuna mpakistani mwenye duka makoroboi,lumumba,karuta wala rwagasore
    so wewe ni mbaguzi tu inachatakiwa ni watu kuishi kwa amani na upend
    MUNGU IBARIKI MWANZA MUNGU IBARIKI TANZANIA NA TUEPUSHE NA WABAGUZI HAWA

    ReplyDelete
    Replies
    1. ULIFURAHIA KUPONDWA MSIKITI WA WAHINDI MWANZA, MATOKEO YAKE UNA NINI LA KUSEMA SASA MAKANISA YANASHAMBULIWA.MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU CHUNGU.mWALIMU ALISEMA UKILA NYAMA Y7A BINADAMU ..... NA BADO TUTATOKA KWA WAHINDI THEN WAISLLAMU...THEN WAKRISTO ...THEN WACHAGA NA WAHAYA WAONDOKE MWANZA...MWISHO NINI? UKIFUATILIWA HATA HATA WEWE LABDA UNASTAHILI KUONDOKA KWA MFANO WAJALUO TUTAWASINDIKIZA SUDAN KUSINI NK.
      NANI MWENYE ASILI YA TANZANIA? NANI ABAKI NANI AONDOKE? TUTAIKIMBIA NCHI KWA USHABIKI WA KIPUUZI

      Delete
  4. naungana na kukupongeza mtoa maoni hapo juu,kwanza mimi ni mzaliwa wa karuta na niko masomoni ngambo
    nimeangalia video za vurugu kutoka bermeda tv,na picha katika blog mbali mbali nasema kwa uhakika sijaona hata mtu mmoja wa lumumba,karuta,rwagasore keyata,uhuru, liberty,mtakuja ,sukuma ,mviring ,nera, makayenye,unguja,usumau,pamba. so naamini hao walio leta fujo si wazawa wa mwanza mjini so plz hizo fujo zenu pelekeni igogo nyakato kirumba igoma na kwingine sisi tunachotaka maendeleo ya kibiashara hatuna ubaguzi kila mtanzania ana haki ya kufanya biashara na kufata taratibu za serikali.msilete njaa na siasa zenu mjini

    ReplyDelete
  5. jamani watanzania mmechoka amani , acheni acheni nyie wenye siasa ya chuki na ubaguzi wa rangi na udini . mmekaa kuanzisha vurugu halafu muibe kwenye biashara za watu . ndio mnachokitaka wizi wizi wizi tu.

    ReplyDelete
  6. we uliye sema vurugu zije kirumba umeambiwa kirumba ndo sehemu ya wana vurugu tumia usomi wako kama unaijua mwnaza vizuri usinge sema ulivyo sema. kwanza haupo nchin you dont know what is real happen i n tz una soma na kujionea tu ila hau experience maisha wanayo ishi watu wachini hasa hao wa maching. kama leo marekani wana hali mbaya kwa usomi wako what do u think about tanzania? be cognetive

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.