ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 5, 2011

ASANTE MUNGU KWA KUMNUSURU MWANANGU OBAMA ALIYEMEZA SARAFU YA SH 50

X-ray ya pili.
Ilikuwa ni asubuhi ya Jumatatu ya tarehe 27juni2011 nikiwa na plani za kuamka saa 3 mara baada ya uchovu wa pilika pilika za siku iliyopita yaani Fiesta Mwanza stimu za usingizi zilikatika ghafla mara baada ya mke wangu kunipa taarifa kuwa my second kid Cuthbert aka Obama(3) kameza sarafu ya shilingi 50.

Huduma ya kwanza ilikuwa nikumuuliza yu hali gani na anajisikiaje:
Jibu: "nimemeza hela kama wali"
Swali: iko wapi?
Jibu: "nimetupa humu.." akielekeza kidole mdomoni
Swali: sasaaa.. huumiii?
Jibu: "mmh-mmh" akimaanisha kukataa

Ndipo pilika zikaanza kutafuta daktari ambaye alishauri kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi. Tulipita hospitali kadhaa bila mafanikio nyingi zikiwa hazitoi huduma ya X-ray kutokana na tatizo la mgao wa umeme linaloendelea nchini.

Huku na huko hatimaye tuakapata huduma ya X-ray katika hospitali binafsi inayoitwa 'Mwananchi' iliyoko wilaya ya Nyamagana mitaa ya Makoroboi nayo ikaonyesha sehemu sarafu hiyo ilipofika, madaktari wakasema kuwa ipo katika eneo lisilo la mashaka sana (kwenye utumbo kifuani) hivyo tumrudishe siku ya pili kama hatakuwa ameitoa kwa njia ya haja kubwa.

Siku ya pili X-ray ikafanyika na kuonyesha kama inavyoonekana pichani juu. Nao madaktari wakasema kuwa ipo kwenye utumbo imeshuka kidogo chini ya mbavu hivyo akatupa siku mbili kurejea kama haitakuwa imetoka. Kweli baada ya siku mbili .... Ikatoka.

Ashukuriwe Mola muumba wa mbingu na nchi.

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. Pole sana kaka G, ila Mungu ni mkubwa ndo maana imetoka.Watoto bwana wana hatari sana.

    ReplyDelete
  2. da, ebwana pole sana, manake ilikuwa ni presha tupu inaonekana, pole mkuu

    ReplyDelete
  3. Sengo najua ulipita katika hali tete ila sifa na utukufu ni kwa Mungu Pekee kwa jinsi alivyofanya kumuokoa Obama(cathbert).By Hosanna Inc

    ReplyDelete
  4. nilipata sms kuhusu tukio hilo lisaa limoja baadae kutoka kwa mama Obama kwa ufupi sana kama telegram ikisema"OBAMA KAMEZA SH.50.....
    Muda huo huo nikapiga simu kwa mama Obama ndo akanisimulia ilivyokuwa baada ya kumaliza nikamuuliza Obama yuko wapi kwa sasa?akajibu kuwa yuko nae kwenye gari yuko bize anacheza ngoja nikupe uongee nae

    OBAMA:Shkamoo anko
    MIMI:Marhaba obama,hujambo
    OBAMA:Anko nimemeza helaa

    Yani baada ya hapo nikatamani na mimi kurudia utoto maana Obama alikuwa hana wasi wasi wakati mama yake alikuwa ameshalia mpaka sauti ikawa haimtoki tena na Baba mtu anapiga simu kwa ma-dokta wote ambao anafahamiana nao ili apate ushauri kuhusu tukio hilo.
    Baba mtu kuonyesha kuchanganyikiwa zaidi nilimpigia simu akapokea na kunisalimia kama ifuatavyo
    MIMI:Hellow
    SENGO;Habari dokta?
    MIMI:Kaka mimi ni Edgar hapa
    SENGO:Duh! vipi shem za asubuhi
    MIMI:Salama tu kaka,lakini hivi sasa ni saa nane mchana sio asubuhi Kaka.
    POLENI SANA MR&MRS Sengo kwa hicho kipindi kigumu cha muda mfupi mlichokipitia.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.