Na
Amiri kilagalila-Njombe
Licha
ya uwepo wa changamoto katika utoaji na utekekelezaji wa huduma za afya nchini,taarifa
ya mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya nyanda za juu kusini inaonyesha
utekelezaji mzuri katika usajili wa maduka ya dawa za binadamu mkoani Njombe
huku moja pekee likibainika kuto kuwa na usajili.
Taarifa
ya matokeo ya ukaguzi wa mwezi wa 7
mpaka wa 12 mwaka 2019 iliyosomwa katika kikao cha kawaida cha TMDA na
wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika ukumbi wa chuo cha
afya Kibena, kwa lengo la kuwaongezea uzoefu,inaonesha maduka matatu huku moja
likiwa ni la dawa za binadamu na mawili ni dawa za mifugo hayakuwa na usajili
pamoja na vibali vya kuendesha biashara huku wamiliki wakiagizwa kuomba usajili
wa vibali ndani ya siku 14.
Aidha
Idadi ya majengo ya afya yaliyokaguliwa katika kipindi hicho,kanda ilikagua
jumla ya majengo 128 ikiwa hospitali 12,vituo vya afya 13,zahanati 4,famasi
9,maduka ya dawa muhimu 70,maduka ya dawa za mifugo 19 na maabara 1.
Anitha
Mshighati ni kaimu meneja wa TMDA kanda
ya nyanda za juu kusini,amasema wataendelea kukumbushana na kutoa elimu ili
kuepusha ukiukwaji katika utoaji huduma.
“Tunataka
kuhakikisha vile vitu ambavyo tumevisajili vinaendelea kuwepo sokoni na katika
ubora ule ule maana sio kila wakati wakaguzi wanakuwepo wakati wa uhishaji wa
bidhaa,kwa hiyo tunatakiwa kuhakikisha ubora tulioukubali unaendelea kuwepo
katika nchi yetu”alisema Anitha Mshighati
Mganga
mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Bumi Mwamasage amesema ukaguzi hufanyika kila robo
ya mwaka katika maduka yote ya dawa mkoani Njombe licha ya kuwepo kwa
changamoto za ukiukwaji wa sheria huku hatua za kisheria zikiendelea
kuchukuliwa kwa wanaobainika.
Katalina
Revocati ni katibu tawala wa mkoa wa Njombe,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
kikao hicho,ametoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri zote kuendelea kutekeleza
majukumu ya udhibiti wa bidhaa za afya ili kulinda afya ya jamii.
“kumekuwa
na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikijitokeza ambazo sisi sote
tunatakiwa kuwa walinzi maswala haya ni kama vile halmashauri kuto kufanya
kaguzi za mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma za afya na maduka ya
dawa,kufuatilia dawa na vifaa tiba,hali hiyo inasababisha baadhi ya maduka na
vituo vya afya kuendelea kuhifadhi dawa katika mazingira yasiyofaa hivyo
kuhatarisha ubora wake”alisema Katalina Revocati
Baadhi
ya washiriki katika kikao hicho wamekiri kupokea mafunzo na kwenda kuyatumia
kikamilifu ili kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa jamii.
Kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini,Anitha Mshighati akiendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu/watendaji wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha afya Kibena mjini Njombe mkoani humo.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa makini kusikiliza,wakati wa kikao cha
afya kilichofanyika mjini Njombe.
Katalina
Revocat katibu tawala wa mkoa wa Njombe aliyekuwa mgeni rasmi akitoa hotuba ya
ufunguzi wa kikao cha wataalamu wa afya na TMDA kilichofanyika katika ukumbi wa
chuo cha afya kibena.
Kaimu meneja wa TMDA
kanda ya nyanda za juu kusini, Anitha Mshighati wakati alipokuwa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
Dkt.Bumi
Mwamasage mganga mkuu wa mkoa wa Njombe akizunguzmza na waandishi wa habari
mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi iliyotolewa kwa wataalamu wa afya na
mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya nyanda za juu kusini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.