ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 8, 2024

YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


WENYEJI, MC Alger wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.

Mabao ya MC Alger yamefungwa na beki Ayoub Abdellaoui dakika ya 64 na mshambuliaji Soufiane Bayazid dakika ya 90'+5.

Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga ambayo ilianza michuano hiyo vibaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Hilal nyumbani, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wakati MC Alger inapata ushindi wa kwanza kufuatia isare ya bila mabao ugenini na TP Mazembe Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mchezo mwingine wa Kundi A utafuatia Jumapili usiku, Al Hilal Omdurman watakuwa wenyeji wa TP Mazembe kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott, Mauritania.​

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.