HABARI NA VICTOR MASANGU, PWANI SAUTI NA ALBERT G.SENGO Naibu katibu mkuu Wizara ya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amewataka watumishi wa sekta ya elimu kufanya kazi kwa weredi na kuhakikisha wanatumia nafasi zao kwa maslahi ya umma ikiwa pamoja na kutumia vikao mbali mbali kwa ajili ya kutoa ushauri ambao utaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kuimarisha misingi ya uongozi pamoja na utawala bora. Hayo ameyabainisha wakati wa halfa ya mahafali ya 32 ya wakala wa maendeleo ya uongozI wa elimu (ADEM) ambapo amewahimiza wahitimu 998 waliomaliza mafunzo ya kozi mbali mbali kuhakikisha wanakwenda kuyaatumia vizuri kwa lengo la kuweza kuchochea maendeleo katika sekta ya elimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.