ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 4, 2014

HILI NDILO PICHA KAMILI NA TAARIFA YA MAFURIKO YALIYOTOKEA MWANZA.

MVUA kubwa iliyonyeesha juzi (jumanne) asubuhi imeleta mafuriko katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza  huku eneo la mabatini likiathirika zaidi na mafuriko hayo yaliyoambatana na mvua kubwa iliyonyeesha takribani  kwa muda usipoungua  masaa mawili.

Mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika nyumba za wakazi wa maeneo ya mabatini,pia mafuriko hayo yalisababisha magari kutopita eneo la daraja la mabatini linalotumiwa na waenda kwa miguu baada ya maji hayo ya mafuriko kuigawa barabara ya mabatini hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano.

Juhudi za jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao walifika mapema eneo la tukio zilisaidia kuokoa baadhi ya wakazi wa nyumba zilizokumbwa na mafuriko yaliyosababisha nyumba hizo kujaa maji ndani.
Katika zoezi hilo la uokoaji watu mbalimbali waliokolewa wakiwepo watoto wadogo na akina mama huku mali mbalimbali zikiwemo runinga,vitanda,magari yakisombwa na mafuriko hayo.
Akizungumzia tathimini ya zoezi nzima la uokoaji Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Jijini Mwanza,Andrew James Mbate amesema zoezi la uokoaji lilienda vizuri na walifanikiwa kuokoa maisha ya watu waliokowepo ndani ya nyumba huku akitanabaisha changamoto mbalimbali walizokutana nazo katika zoezi zima. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Wanajeshi wa Kikosi cha zimamoto Mwanza wakimvusha mama huyu kutoka juu ya paa la nyumba moja hadi upande wa pili penye usalama kupisha maji yaliyokuwa yamefurika hata kuzifunika nyumba za wananchi eneo la Mabatini jijini Mwanza. 
“Zoezi la uokoaji lilienda limeenda salama na linaendelea vizuri tunashukuru wenzetu wa shirika la umeme waliwahi kukata umeme mapema hali iliyopelekea sisi kama Jeshi kuanza kazi mara moja tulivyofika eneo la tukio”. Aliongeza Gadafi ambaye ni msemaji wa jeshi la Zimamoto

Akizungumza juu ya mafuriko hayo mkazi wa mabatini,Charles Samson alisema wamepoteza vitu vyao vya thamani huku wakioomba serikali iwasaidie kuhama mabondeni kwani madhara yaliyowakuta ni makubwa.

Tanesco walizima umeme kwaajili ya tahadhali.




Kivuko asilia ni ajira kwa wengine.
Gari hili nyang'anyang'a mara baada ya kusombwa na mafuriko na kubinuliwa kisha kutoswa mtaroni. 
Msaada tutani.
Eneo la mabatini ni eneo ambalo mto mirongo unapita hali iliyosababisha mafuriko hayo kuwa makubwa kwa kuwa maji yam to huo yanatoka sehemu mbalimbali za wilaya zilizopo Mkoani Mwanza ikiwemo wilaya ya magu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.