NA. Mwandishi wetu
Musoma.
POLISI mkoani Mara wamelazimika kutumia mabomu
kuwatawanya wafuasi wanaotajwa kuwa niwa Chama cha maendeleo na demokrasia
nchini CHADEMA waliokuwa wakimfanyia fujo aliyekuwa mbunge wa zamani wa Musoma
mjini Bw. Vedastus Manyinyi Mathayo wa CCM.
Mathayo ambaye pia alikuwa mjumbe wa NEC
inatajwa kuwa amefanyiwa vurugu hizo leo wakati alipokuwa akishiriki kuhani
msiba wa aliyekuwa Sheikhe wa Musoma Othman Magee aliyefariki dunia juzi
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipelekwa kwaajili ya kupatiwa
matibabu mara baada ya kuhamishiwa toka hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza
ambapo ilishindikana.
Taarifa zinasema kuwa mara baada ya
Mkutano wa hadhara wa CHADEMA kumalizika wanachama wa chama hicho wakiwa
wameambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Wilbrod Slaa pamoja na mbunge
wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere walielekea kwenye msiba kwaajili ya
kujumuika na wafiwa na wananchi wengine.
Wanachama hao walipofika kwenye msiba huo
na kumkuta mbunge wa zamani Musoma mjini Bw. Mathayo walianza kumshambulia kwa
maneno na katimaye mawe huku wengine wakiburuta pikipiki zao na kulifanya eneo
hilo kuwa na hali tete hata baadhi ya magari yakipondwa mawe kwenye eneo la
msiba huo.
Dakika chache baadaye polisi walifika
katika eneo la msiba ambalo lilikuwa si tulivu tena na kujaribu kuituliza hali
kwa njia za kidiplomasia na iliposhindikana walilazimika kurusha mabomu ya
machozi ili kupata kuwatawanya wafuasi hao.
Marehemu Sheikh Othman anatarajiwa kuzikwa
kesho mjini Musoma.
Taarifa zaidi kuwajia:- ITAENDELEA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.