ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 23, 2014

WAMILIKI 10 WA MADUKA BUBU WAKAMATWA WAPANDISHWA KIZIMBANI KATI 100 MSAKO KUENDELEA JIJINI MWANZA

NA PETER FABIAN.
MWANZA.


WAMILIKI wa maduka bubu ya dawa baridi wapatao 10 kati ya 100 waliokamatwa kufatria operesheni maalumu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mukazi Wilaya ya Nyamagana kwa kosa la Jinai jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mahakamani hapo mwishoni mwa juma lililopita, mmoja wa wanasheria kutoka Jiji la Mwanza, Alhaj Bwabo Makusudi alisema kwamba watuhumiwa hao 10 waliopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ya kosa la jinai mahakimu wawili tofauti wa Mahakama hiyo.

Makusudi alifafanua kukamatwa kwa watuhumiwa hao kati ya 100 kulitokana na zoezi la ukaguzi na operesheni maalumu iliyofanywa na kikosi kazi cha pamoja cha Halmashauri ya Jiji, Manispaa ya Ilemela na Idara zingine za serikali ambapo watuhumiwa 10 awali walifungiwa maduka yao lakini waliyafungua na kuendelea na utoaji huduma nyakati za usiku kabla ya kukamatwa tena.

Aliwataja watuhumiwa hao kumi waliopadishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mbele ya Mahakimu, Ainawe Moshi na Janeti Masesa wa Mahakama hiyo, kuwa ni watuhumiwa James Warioba (30) mkazi wa Butimba, Likutuye Paschal (30) mkazi wa Mkolani, Amayo Joshua (29) mkazi wa Igoma, Issa Kubona (58) mkazi wa Igoma (wote Nyamagana) na Neema Kitinya (45) mkazi wa Kisesa (Magu).

Wengine waliopandishwa kizimbani ni Fatuma Martine (24) mkazi Kilimahewa,  Wangeta Musanya (25)  mkazi wa Butimba , Anna John (50) Uzinza (wote nyamagana na Maua Ally (23) mkazi wa Kiloleli (Ilemela) ambapo wakipatikana na hatia watapewa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jera au kutozwa faini isiyozidi milioni 10.

Makusudi alisema watuhumiwa wengine 100 baadhi yao wametozwa faini na wengine wanaandaliwa mashitaka ili kufikishwa mahakamani kulingana na makosa waliyokamatwa nayo wakati wa utekelezwaji wa zoezi hilo linaloshirikisha Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Jiji la Mwanza, Edward  Magelewanya , alisema kwamba hatua ya kuwafikisha mahakamani inatokana na watuhumiwa hao kukamatwa katika zoezi la ukaguzi na operesheni iliyofanywa tangu Desemba 8 hadi 20 mwaka katika maeneo yote ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Magelewanya alisema kwamba lengo kuu la ukaguzi na operesheni hiyo iliyofanywa katika maduka 171 na kikosi kazi kikihusisha Idara Afya za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela na zingine za serikali, ilikuwa na lengo la kuangalia kama sheria, kanuni, miongozo, viwango na taratibu za kutoa dawa kwa sekta binafisi zinafuatwa , zinatekelezwa na wamiliki na wanaofanyabiashara hiyo.

Alifafanua kuwa zoezi hilo pia lililenga kujilidhisha kuona kama wamiliki wana vibali kutoka Baraza la Famasi Tanzania, Leseni za biashara, Usajili wa majengo na Ubora wake, kufatilia Watalaamu wanaotoa huduma kwa walaji wa dawa kama wanakidhi vigezo na wanatambuliwa na Baraza la Phamacy’s nchini, kufatilia uwepo wa dawa za serikali katika sekta binafsi.

“Utekelezaji wa zoezi hili pia ulilenga kuchukua hatua sitahiki, kuangalia nyaraka muhimu za utendaji kazi katika maduka hayo ya watu binafsi na vitabu vya rejea na kufatilia majengo nyanayoendesha huduma hii kama yanakidhi vigezo vinavyotakiwa katika kuhifadhi dawa na kutoa huduma , ” alisisitiza na kuongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Magelewanya alisema kuwa zoezi hilo limeshirikisha Ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa, Waganga Wakuu wa Wilaya za Nyamagana na Ilemela, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkoa, Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa, Maafisa Biashara wa Mkoa na Halmashauri zote mbili, Ofisi za Mfamasia wa Jiji na Manispaa ya Ilemela na Vyombo vya Ulinzi na Usalama na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.