ASKOFU Mkuu wa Kanisa la African Inland Charch Tanzania (AICT),Dayosisi ya Mwanza John Bunangwa, amewataka waumini kuliombea Taifa la Tanzania kwa Bwana Yesu ili kuliepusha kuingia kwenye dhambi na machafuko yanayoweza kuliangamiza.
Askofu Bunangwa akizungumza jana na waumini wa kanisa la AICT Makongoro Dayosisi ya Mwanza, alisema waumini na watanzania wote kwa ujumla bila kujali madhehebu yao na itikadi zao bali wanao wajibu mkubwa wa kuliombea Taifa kwa Bawana Yesu ili kuliepusha kuingia kwenye machafuko na dhambi ambayo inaweza kuleta vurugu na kutoweka kwa amani na utulivu uliopo sasa.
"Kuna baadhi ya watu wamekuwa waongo na wamewaiga Adamu na Eva waliomdanganya mungu na kutumbukia kuchuma dhambi ambazo leo hii wamejitumbukidha na kumsahau Bwana Yesu na kufanya vitendo vinavyomchukiza Mungu,"alisema.
Askofu, amewataka watanzania kuendelea na maombi na sala za kuliombea Taifa ili kuepuka kufika mwaka 2015 tukiwa tumejitumbukiza kwenye dhambi ya Adamu na Eva na kupelekea kuingia taifa kuwa kwenye machafuko na kusababisha amani na utulivu kutoweka na kuanza kusambaratika, hivyo ni vyema tukaendelea kuomba na kusali katika makanisa na majumbani kwetu.
"Niombe wenye dhambi mlioko humu kanisani mpite mbele ili kutubu na kuomba kusamehewa dhambi kwani dhambi ni usaliti kama wa Adamu na Eva ili msiende majumbani mwenu kusherehekea Chrismas mkiwa na dhambi bali muende mkiwa wasafi na wenye matumaini makubwa,"alisisitiza
Amwataka waumini kuwa na utaratibu wa kutubu kwani ni kubadilika kifikira na kuwa na mwenendo mzuri kwa kila muumini na mwananchi wa taifa hili jambo ambalo kwa kila mmoja akilitekeleza kwa vitendo kutasaidia kuwa Taifa lenye kumpendeza mungu siku zote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.