Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa.
Mkazi wa kijiji cha Kibitilwa kata ya Ilula
Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Marko Samwel (32) anatibiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Kanda ya Bugando chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi baada ya kujikata
na kuondoa kabisa uume wake kwa kutumia kisu.
Samwel anadaiwa
kujifanyia kitendo hicho cha kikatili Mei 3 mwaka huu Saa 7 usiku kwa madai
kuwa amechoka kuuguza maradhi yanayomsumbua (yamehifadhiwa) kwa zaidi ya miaka
mitano.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema mwanaume huyo alijikata kwa kutumia
kisu kisha kuziondoa kabisa sehemu zake za siri jambo lililosababisha apoteze
damu nyingi na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba kabla yakupatiwa rufaa
ya kwenda Bugando anakoendelea na matibabu.
"Amekata
uume wake kwa kisu kikali kwa madai kwamba amechoka kuugua, akakimbizwa
Hospitali ya wilaya ya Kwimba lakini hali yake ikazidi kuwa mbaya akakimbizwa
Bugando,"
"Hali yake
inaendelea vizuri na sisi tunaendelea kumsubiria apone kabisa arejee kwenye
utimamu wake ili atueleze kwa nini amekata sehemu zake za siri baada ya hapo
tutamfikisha Mahakamani," amesema Mutafungwa
Mutafungwa
ameitaka jamii kuepuka kuchukua maamuzi yanayoweza kuwaathiri kimwili na
kisaikolojia akitolea mfano tukio hilo na kuwataka wenye changamoto kuwahusisha
ndugu, wanasaikolojia na viongozi walioko katika maeneo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.