ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 12, 2023

MBUNGE KOKA ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUBORESHA SHULE YA SEKONDARI VISIGA.

 

Na Victor Masangu,Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu amechangia mifuko 100 ya sarufi kwa lengo la kukarabati miundombinu chakavu ya madarasa Saba katika shule ya sekondari Visiga.


Koka ametoa ahadi ya kuchangia mifuko hiyo wakati wa halfa inayojulikana Kama Visiga day ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuweka mikakati ya kujadili namna ya kuongeza kiwango cha ufaulu pamoja na kukutana na wazazi ili kujadili changamoto zilizopo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Aidha Mbunge huyo pamoja na kuchangia mifuko hiyo ya saruji ameahidi kuchangia madawati 50 kwa lengo la kuweza kusaidia Wanafunzi kuondokana na changamoto ya kusoma kwa mlundikano.


"Kikubwa natambua elimu ndio kila kitu kwa hivyo nimesikiliza risala ya mwalimu mkuu na nimegundua kuna mahitaji ambayo yanatakiwa katika kukuza kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi na kuondokana na adha ya kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki,"alisema Koka.

Kadhalika Mbunge huyo aliongeza lengo lake kubwa ni Kuhakikisha anashirikiana bega kwa bega na wazazi,walezi pamoja na walimu katika kuwalinda Wanafunzi katika kuwa na nidhani ya kusoma kwa bidiii ili kuondokana kabisa na kupata alama mbaya.

"Kunatakiwa walimu,walezi na wazazi kwa pamoja tushirikiane katika kuwasaidia Wanafunzi wetu ili kutokomeza zero kabisa katika shule hii ya Visiga sekondari na kwamba anachukukizwa na shule za kata kuitwa kayumba,"alisema Koka.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Visiga Abasi Kikonyo katika risala yake amemshukuru Mbunge kwa sapoti yake ya kuisaidia shule hiyo pamoja na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo wazazi sambamba na viongozi wa chama kwa kuchangia michango na vifaa vya ukarabati wa madarasa.


Naye Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwajuma Nyamka amesema Mbunge huyo anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo hivyo anastahili kuungwa mkono katika kuchochea maendeleo.


Nao baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo hawakusita kutoa pongezi zao za dhati katika kuona umuhimu mkubwa wa kusaidia ukarabati wa madarasa pamoja na kuchangia meza na viti ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa wa kusoma kwa mlundikano.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.