Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa (wapili kutoka kulia) akikata utepe wa kuashiria uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa madhehebu ya Kikristo Mwanza, kulia ni askofu wa Kanisa la Anglican Diosisi ya Nyanza (DVN) Boniface Kwangu akiwa ameshikilia kiasi cha shilingi millioni 40 zilizochangwa ikiwa ni pamoja na hudhi na ahadi zilizowekwa kutunisha Vikoba, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti pia anaonekana pichani wa pili kushoto . |
Na Albert Sengo.
WAZIRI Mkuu Mstaafu
Edward Lowassa amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Zanzibar Dkt.Mohamed Sheni kwa njisi
ambavyo wamekuwa wakikazia suala la kudumisha amani nchini, wakiwemo viongozi
wa Taasisi za kidini Kalidinali, Askofu Mkuu Polycarp Pengo (Romani),Askofu
Alex Malasusa (KKKT), Mufti Shekhe Mkuu wa Tanzania Simba Bin Simba na
viongozi wengine wakiwemo wachungaji wa madhehebu mbalimbali nchini.
Lowassa alitoa pongezi
hizo leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa
Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela uliofanyika katika
Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela na kueleza
kwamba viongozi hao wamekuwa wakikemea udini na kutaka watanzania kuendelea
kuilinda amani ya nchini kama mboni ya jicho kwani kuipoteza Amani tuliyonayo
nchini itatugharimu maisha kuirejesha hivyo amewasihi watanzania wasichoke na
Amani ambayo ni kama hewa ikitoweka haiwezi kurudi tena kamwe.
Hatimaye maandamano yalifika katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela. |
Kwaya ya Anglican Nyamanoro Mwanza nayo ilihudumu kwenye ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. |
Ibada ya maombezi ikiendelea kanisani. |
Aidha Mbunge huyo wa Jimbo la Monduli na Mjumbe wa NEC CCM Taifa wa Wilaya ya Monduli amewataka wanasiasa wote nchini kumuunga mkono kuiomba serikali kurudisha fedha za Mabilioni ya JK na kuhakikisha yanapelekwa moja kwa moja kwa wanawake wa vijijini walioanzisha VICOBA ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi hali ambayo itawawezesha wanawake wengi kuondokana na umasikini.
Sikiliza alichosema..
Utaifa zaidi ndani ya kwaya ya kanisa la DVN. |
Aidha amewataka watanzania wote kuwasikiliza viongozi
hao na kuwaunga mkono katika kukemea watu wanaotaka kuwatuawa na kusababisha vurugu ili amani tuliyonayo
nchini iweze kupotea kwa masilahi yao kamwe wasikubali hivyo ni vyema wakaungana
kuwakataa kwa nguvu zote kwani hadi sasa wagombea Urais wan chi ya Kenya
wanawataka wakenya kuwa kama watanzania hivyo hivyo na Waganda wamekuwa
wakihubiliwa kutuiga kutokana na umoja na amani tuliyonayo hapa nchini.
Furaha ya mchungaji na mwanae. |
Furaha. |
Saa 6:30 mchana shughuli ya uzinduzi inamalizika na Mh. Lowassa anaondoka eneo la tukio huku akipeana mkono na waumini. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.