ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 6, 2024

MAMA KOKA AUNGANA NA RAIS SAMIA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU SHULE YA MSINGI BOKO TIMIZA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka aunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta  ya elimu  ameahidi kuchangia viti na meza kwa ajili ya walimu wa shule ya msingi Boko Timiza.

Mama Koka  ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe ya mahafali kwa wanafunzi wa liohitimu darasa la saba katika shule ya msingi Boko Timiza iliyopo Kata ya Tumbi Wilaya ya Kibaha.

Mama Koka amesema kwamba licha ya kuahidi kuchangia viti na meza pia amechangia matofali  500 kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule.

"Nimesikia risala yenu na mimi kama mke wa Mbunge  nipo pamoja na nyinyi na nitasaidia viti na meza pamoja na matofali 500 ambayo yatasaidia katika mradi unaondelea wa madarasa.
Aidha Mama Koka amesema Mbunge anatambua elimu ni ufunguo wa maisha hivyo ataendelea  kushirikiana bega kwa bega katika kuiboresha zaidi shule ya msingi Boko Timiza ili iwe katika mindombinu  mizuri.

Kadhalika aliwahimiza wazazi na walezi kuwalinda na kuwatunza watoto wao ikiwa pamoja na kuwapatia malezi bora,maadili pamoja na kuwapatia mahitaji mbali mbali ya msingi.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo  Ramadhani Mfinanga amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Pia amemebainisha kwamba  kwa sasa shule hiyo ambayo imeanzishwa mnamo mwaka 1978 ambapo kwa sasa  ina jumla ya ya wanafunzi wapatao 75 ambapo ina madarasa 7 kwa ajili ya kusomea wanafunzi.



Naye  mmoja wa wanafunzi katika shule hiyo  Nuru akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake amebainisha kwamba bado shule hiyi inakabiliwa na changamoto ya madarasa ikiwa pamoja na uhaba wa matundu ya vyoo.

Shule ya msingi Boko Timiza ambayo ipo katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha mjii  imeanzishwa tangu 1978 lakini  bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinahitajika juhudi za makusudi katika kuzitafutia ufumbuzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.