ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 11, 2018

KAMANDA SHANNA AONGEZA NGUVU VITA YA UBAKAJI NA VITENDO VYA UKATILI MISUNGWI.



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

WANAWAKE wilayani Misungwi mkoani Mwanza wameliomba jeshi la polisi kukomesha vitendo vya kinyama dhidi yao ikiwemo kukatwa sehemu za siri na kisha kuuawa ambavyo vimechangia baadhi yao kuishi kwa hofu.
Wakizungumza wakati wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani humo, baadhi ya wanawake wamesema kuwa vitendo vya kikatili dhidi yao vimesababisha wengi wao kushindwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kujipatia kipato kutokana na hofu ya kuuawa.
Akijibu hoja ya suala la uhakika wa usalama, Kamanda wa polisi mkoa Mwanza JONATHAN SHANA amesema ili kuonesha kuwa Jeshi hilo limedhamedhamiria kuisafisha jamii, tayari mtuhumiwa aliyekuwa akijihusisha na vitendo vya kinyama dhidi ya wanawake na kuwauwa tayari ametiwa mbaroni.
“Mimi kama kamanda wa mkoa wakati yeye anahitimisha mimi nakuja kuzindua kampeni  ya Kupambana na wakatili wa Kijinsia”

“Kama mnavyojua kawaida yangu na kama mlivyokuwa mkiniona mimi nimekuwa nikitoa dakika sifuri tu, pale inapohitimishwa kazi basi mimi ndipo ninapoanza”
“Hivyo nitaanzanao hukuhuku Misungwi”
“Kama wewe umekuwa ukiendeleza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ninapomaliza kuongea hapa, wewe useme Ukatili sasa Basi” Amesema Shanna.

Kampeni ya wiki nane ya kutokomeza ukatili wa kijinsia imeleta matokeo chanya katika wilaya MISUNGWI kufuatia baadhi ya wanaume kuanza kutumia fedha za mauzo ya mazao kwaajili ya maendeleo badala ya matumizi ya anasa. Aidha kampeni hiyo imesaidia kupunguza mimba za utotoni pamoja na utoro.
Kampeni hiyo imetekelezwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la KIVULINI.
Diwani wa viti maalum tarafa ya inonelwa OLIVER MICHAEL akaliomba jeshi la polisi kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.
Awamu ya kwanza ya Kampeni hiyo imehitimishwa katika kata ya NHUNDULU na mkuu wa wilaya Misungwi JUMA SWEDA


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.