ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 12, 2018

AJIUWA KWA KUJIRUSHA TOKA GHOROFANI.


Mapema Leo asubuhi mtu mmoja aliyetambulika kama Afisa Usimamizi wa fedha nchini Kenya (PriceWaterhouseCoopers (PwC)) amefariki dunia baada ya kujirusha ghorofani toka kwenye  moja ya majengo mjini Nairobi.

Bwana huyo anakwenda kwa jina la Stephen Mumbo, Meneja msaidizi wa PwC. 

Mkuu wa polisi wilaya ya Kilimani mjini Nairobi Michael Muchiri amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Alikuwa Meneja Msaidizi wa Upelelezi wa Uendeshaji na Ushauri wa Kitaifa katika kampuni,” Amesema Muchiri . 

Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza, ripoti zinaonyesha kuwa Mumbo alikimbizwa Hospitali ya Aga Khan ili apatiwe matibabu ya huduma ya kwanza lakini alishindikana kutokana na majeraha yake kuwa makubwa


Bado haijulikani nini kinachoweza kumchochea kuchukua hatua hiyo ya kukatisha maisha yake yeye mwenyewe

#PWC #PriceWaterHouseCoopers #Suicide #Kenya #BreakingNews 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.