NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Wananchi wa jimbo la
kwimba mkoani Mwanza, wamempongeza mhe.Shanif Mansoor, mbunge wa jimbo la
kwimba, kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo wakazi wa kata ya shilembo kwa
kuwafungulia barabara zaidi ya km.30 kwa kutumia posho ya mshahara wake.
Diwani wa kata ya
shilembo mhe.Elias Garula, amesema zaidi ya miaka 5o tangu vijiji hivi
viazishwe hawakuwahi kuona barabara wala gari katika maeneo hayo, wananchi
wamesema kutokana na changamoto ya barabara, wanawake wengi wamepoteza maisha
na watoto hasa wakati wakujifungua, kutokana na ukosefu wa miundombunu ya
barabara ambapo magari yalishindwa kufika katika vijiji vya shilembo.
Wananchi wamempongeza
MANSOOR, kwa jitihadazake binafsi za kuwafunguliya barabara hiyo,ambazo kwao
ilikuwa ni ndoto kwani maendeleo yamechelewa kufika maeneo hayo kutokana na
changamoto ya kukosekana kwa barabara.
Ndalawa Magashi, ni
mtendaji wa kata ya shilembo tarafa ya mwamashimba wilayani kwimba mkoani
Mwanza, amema,shukuru kubwa kwa mhe.MASOOR,kwa kazi nzuri anayo ifanya kwa
wananchi wa jimbo la kwimba, nakusema wabunge wengi wamepita kwenye jimbo la
kwimba lakini MANSOOR,ni mbunge wa pekee, maarufu mbunge wa vitendo.
Aidha wanancha wa kata
ya shilembo baada ya kuona Greda limefika katika kata hiyo,walionyesha furaha
yao huku wakipiga kelele za vifijo na nderemo kwakuona greda limeanza kuchimba
barabara hiyo, kwani wanafunzi pia kipindi cha masika wanapatashida kuvuka
maeneo korofi na wengine kushindwa kuhudhuriya masomo.
Pia wananchi wa kata
shilembo, wameomba serekali kuangalia barabara hiyo kwa jicho la tatu kuiwekea
moramu na kalavati ili barabara hiyo iwe ya kudumu na endelevu, kwani itafungua
maendeleo katika maeneo hayo vijiji vya shilembo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.