Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza na wanachama wa chama cha Tuungane wakulima Interpises katika kijiji cha Mbugani kilichopo kata ya Itunundu Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mpunga katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashamba ya mpunga alipotembelea Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua Ghala la kuhifadhi mpunga la Tuungane Wakulima Inteprises wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashine ya kukoboa mpunga ya Chama cha Tuungane Wakulima Inteprises wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.
Na Mathias Canal-WK, Iringa
SERIKALI imesema itahakikisha mbolea inawafikia
wakulima kwa wakati kabla ya kuanza msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 kwani
umuhimu wa mbolea ni pale inapowafikia wakulima shambani sio kuhifadhiwa ghalani.
Katika msimu ujao Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima
wanapata mbolea na pembejeo nyingine katika maeneo yao wakati wote wanapohitaji
ili kuondoa adha ya muda mrefu ya mbolea kuchelewa kuwafikia wakulima kwa
wakati.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba ametoa kauli hiyo leo
tarehe 12 Octoba 2018 wakati akizungumza na wanachama wa chama cha Tuungane
wakulima Interpises akiwa katika ziara ya kikazi kata ya Itunundu Mkoani Iringa
kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Dkt. Tizeba amesema kuwa ili kuboresha usambazaji wa pembejeo kwa
wakulima katika msimu wa mwaka 2017/2018 mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja
(Bulk Procurement system- BPS) umeongeza upatikanaji wa mbolea kwa wingi, bei
nafuu na wakati.
Aidha,
kwa kutumia utaratibu huo bei za mbolea aina ya DAP na UREA zimepungua kwa
wastani wa asilimia 30.
Akifafanua zaidi, Dkt Tizeba alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa
Mbolea (TFRA) inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na pindi ukiukwaji wa
bei elekezi unapobainika hatua stahiki zinachukuliwa kwa wahusika.
” Endapo kama kuna mtu atapandisha gharama za mbolea kwa kupandisha
bei maradufu zaidi ya bei elekezi serikali itamchukulia hatua haraka za
kisheria atakayebainika ” Alikaririwa Dkt Tizeba
Katika kuimarisha sekta ya kilimo serikali imekuwa ikichukua hatua
mbalimbali kuimarisha kilimo kwa kuwekeza katika pembejeo, mbolea na zana
zinazoweza kuikuza sekta ya kilimo ili iweze kuchochea uchumi wa viwanda.
Kadhalika,
Waziri Tizeba amewatoa hofu wakulima nchini kuwa kuna akiba ya mboleaya awali
isiyopungua Tani 80,000 kwa ajili ya kupandia.
MWISHO
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.