NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtv
JESHI la polisi mkoa wa Mwanza limekamata watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi wakitajwa kuiba gari lenye namba T 929 DCD aina ya HINO mali ya kampuni ya Sanu East Africa LTD ya Jijini Dar es salaam katika eneo la Kishiri - Igoma wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mkoani hapa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema ukamataji huo umefanyika tarehe 11/10/2018 majira ya saa Kumi na Moja jioni. hii ni baada ya Jeshi lake kupata taarifa za kutoka kwa wasamaria wema, wazalendo wakipenyeza taarifa kwamba, kuna watu wameingia mkoani kwake na gari waliloliiba jijini Dar es salaam ambapo mara baada ya taarifa hiyo, Polisi walianza ufuatiliaji wa chocho kwa chocho na hatimaye kufanikiwa kukamata wezi hao wakiwa na gari hilo.
Kabla ya kukamatwa kwa gari hilo, taarifa zinaeleza kuwa ni mara mbili lilipelekwa kwenye gereji tofauti tofauti jijini hapa kwaajili ya kukatwakatwa vipande ili liuzwe kama spea na vyuma chakavu lakini ilishindikana mara baada ya wamiliki wa gereji hizo kukataa kufanya zoezi hilo kutokana na kuwa na maswali mengi yaliyokosa majibu yaliyozingirwa na hofu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.