ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
HATIMAYE wafanyabiashara waliokuwa wakifanya bishara zao katika eneo la kiwanja cha soko dogo la Sahara wamekubali kuliachia eneo hilo kuendelea na matumizi yaliyopanga na mwekezaji wake.
Mathias Charles Ndetto ndiye mmiliki halali wa kiwanja hicho namba 195 A BLOC U Rwagasore anasema amepata faraja kuona muafaka unapatikana na wafanyabiashara hao wanaondoka sasa kwa amani, tofauti na vile ilivyokuwa ikidhaniwa kwama 'pangechimbika'.
Halmashauri ya jiji pamoja na Serikali ya Mtaa baada ya kufanya ukaguzi na uhakiki kwa mabanda katika eneo la Serikali lililopo jirani na kiwanja hicho wamewapanga upya wamachinga kwenye maeneo yao huku wakilazimika kuzifunga baadhi ya njia ndogo za kupita wateja ili kuwapa nafasi wafanyabishara waliohamishwa nafasi ya kupanga biashara zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.