ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 13, 2018

MTUKUFU DKT. SYEDNA MUFADDAL SAIFUDDIN SAHEB AMALIZA ZIARA YAKE JIJINI MWANZA.



GSENGOtV

Octoba 12, 2018 Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS) hatimaye amemaliza ziara yake ya siku 3 mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amemsindikiza Kiongozi huyo katika uwanja wa ndege jijini hapa.


Akiwa na msafara wake wenye watu takribani 25, kiongozi huyo amemaliza ziara yake kwa mafanikio, ambapo aliweka kambi yake ya mapumziko katika eneo la kitalii la Wag Hill Lodge liliyoko Luchelele wilayani Nyamagana.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akimkabidhi  zawadi  Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb picha ya kuchora ya ukutani yenye kuonesha mazingira ya jiwe la utalii lililoko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria eneo la Kamanga, (Bismarck Rock) kama ishara ya kumbukumbu ya ziara yake mkoani hapa.

Ziara ya kiongozi huyo ililenga kutoa baraka kwa waumini wa Jumuiya ya Bohra, kushiriki nao ibada sanjari na kujionea hali ya mazingira ya kiutalii na vivutio vilivyopo mkoani Mwanza, adhma iliyotimizwa bila kukosa hata chembe. 

Mheshimiwa Mongella kamkabidhi Dkt. Syedna zawadi ya picha ya kuchora ya ukutani yenye kuonesha mazingira ya jiwe la utalii lililoko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria eneo la Kamanga, nalizungumzia Bismarck Rock.

Mkoani Tabora ndiko uelekeo wa Kiongozi huyu Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani.
 
"Naaam Picha inazungumza.....Picha imemvutia.........."
Dakika chache kabla ya ndege iliyombeba Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb na msafara wake kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mwanza.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.