NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Onyo limetolewa kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa makosa ya kiuhamiaji kwa kushirikiana na wahamiaji haramu, au kusaidia wahamiaji haramu hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yao. Peter Mbaku ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, ametoa kauli hiyo hii leo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa ripoti ya mwaka wa utekelezaji 2022-2023 ambayo pia aliambatanisha na mipango mikakati iliyowekwa na idara hiyo. Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji yakiwemo makosa ya uhamiaji haramu na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mwaka uliopita 2022 ni watu 783 ambao wanatoka katika mataifa 23. Hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wahalifu na watuhumiwa hao wa makosa ya uhamiaji ikiwemo kufikishwa mahakamani, kuondoshwa nchini, wakimbizi kurudishwa makambini, kupewa onyo kali huku wengine wakiamriwa kushughulikia vibali stahiki na kufanya kazi kulingana na sharia na taratibu za kiuhamiaji. Jeh kwanini wahamiaji hao hupitia mkoani Mwanza? Na nini kinachosababisha watu hao kutoka mataifa mengine kukimbilia nchini Tanzania huku idadi yao ikiongezeka kila uchwao? #mwanza #uhamiaji #wahamiajiharamuTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.