MWANAMUZIKI MAARUFU DR. REMMY ONGARA AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA KUAMKIA LEO KATIKA HARAKATI ZA KUMKIMBIZA HOSPITALI TOKA NYUMBANI KWAKE SINZA JIJINI DAR ES SALAAM. Alipotoa kwa mara ya kwanza kibao kinachoitwa Siku ya Kufa, mwanamuziki Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk Remmy’, akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, wengi walihisi anajichulia kifo chake kiko karibu. La hasha mara baada ya hapo maisha yaliendelea akaishi miaka ishirini naushee.... na hatimaye miaka ya 2004-2005 mzee mzima aliamua kuokoka mara baada kupona toka kuugua sana na hata kupooza. Mwenyewe katika mahojiano nami aliwahi kukiri kuwa Mungu ndiye alimpigania akarejea katika hali nzuri, Remmy aliachana na muziki wa dunia na kuingia ktk fani ya kuhubiri neno la Mungu kwa kutoa album ya nyimbo za injili 'KWA YESU KUNA FURAHA' iliyotumika kubadili wengi. Lakini ndiyo hivyo tena tumeandikiwa kwamba kila kilichozaliwa na mwanadamu hakina budi kufa, hatimaye usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane Remmy Ongala Akaaga dunia wakati akikimbizwa hospitali mara baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Wachezaji maarufu duniani waliokufa kwa ajali
-
Ulimwengu wa kandanda umekumbwa na ajali nyingi mbaya za magari kwa miaka
mingi, zikigharimu maisha ya vipaji vinavyoinuka na wataalamu waliobobea.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.