ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 21, 2026

JKT YATANGAZA NASAFI MAFUNZO YA KUJITOLEA.

news
Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jeneral Hassan Mabena

 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) imetangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa vijana wa Tanzania Bara na visiwani kwa mwaka 2026 huku likisisitiza nafasi hizo ni bure kwa vijana watakaoomba.

Akizungumza katika Makao Makuu ya JKT, Chamwino Dodoma, Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jeneral Hassan Mabena, amesema usahili wa vijana hao utaanza Januari 26 mwaka huu katika mikoa yote ya bara na visiwani.

Amesema utaratibu wa vijana kuomba mafunzo hayo unaratibiwa chini ya ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya na vijana wenye elimu ya kuanzia darasa la saba hadi chuo kikuu wanazo sifa za kuomba, akisema watakaochaguliwa wataanza kujiunga katika kambi mbalimbali za JKT kuanzia February 27 hadi Machi nne mwaka huu.

"Mafunzo haya ni bure wazazi au walezi wasikubali kurubuniwa kutoa fedha ili vijana wao wapate nafasi za kujiunga na mafunzo hayo," amesema Brigedia Jenerali Hassan Mabena.

Amezitaja kozi ambazo wanazipa kipaumbele ni zile za taaluma ya Stashahada ya Teknolojia ya Habari, Stashahada ya Mifumo ya Taarifa za Biashara, Stashahada ya Sayansi ya Kompyuta, Stashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Stashahada ya Usalama Mtandaoni.

Nyingine ni Shahada ya Sayansi katika Sayansi ya Kompyuta, Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari, Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Kompyuta, Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari za Biashara,Shahada ya Sayansi katika Usalama wa Mtandao na Forensics ya kidigitali.

"Nitoe wito kwa Watanzania wenye sifa waende kwenye vijiji kata,tarafa zao ili waweze kujiandikisha, nasisitiza  nafasi hizi haziiuzwi ni fursa iliyotolewa bure kwa Watanzania wote," amesema Brigedia Jenerali Mabena 

Mabena amesema Vijana watakaopewa kipaumbele kuchanguliwa ni waliosoma kozi za masulala ya Sayansi pia akawatahadharisha wazazi kuepuka matapeli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment