Shughuli ndiyo hivyoo imeiva na wageni mbalimbali sambamba na washereheshaji wanazidi kumiminika jijini Mwanza pichani mkali wa hip hop bongo Mwanafalsafa akitinga Mwanza tayari kwa Show ya Serengeti Fiesta itakayo fanyika jumapili hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Nasi tukitinga kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu.
Chiddy Benz nae huyoo akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho Clouds Fm Lovenes love.
Mwana hip-hop Prof J nae ameonekana akiwa mwenye furaha mara baada ya kutua uwanja wa ndege Mwanza kutokea jijini Dar es salaam kwaajili ya shughuli za Fiesta.
Sakafu ya jukwaa. Wasanii wengine wanaotarajiwa kuperform siku hiyo ni pamoja na Mataluma, Barnaba, Linah, Godzillah, Sajna, Diamond, Recho, Makomandoo, Chriss Wamalya, Fid Q na mkali wa muziki wa Dancehall, Ragga & Reggae - Shaggy.
NB: Kuanzia saa sita kamili mchana kila nusu saa droo itachezeshwa na mshindi kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano taslimu, zoezi hilo la zawadi litadumu hadi itakapotimu saa nane mchana "CHANGAMKIA MZIGO HUO MWANAWANE"
TIA YAANZISHA KAMPASI MPYA MKOANI TANGA
-
NA EMMANUEL MBATILO
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeanzisha Kampasi mpya ya TIA mkoani
Tanga, ambayo inalenga kuhudumia wanafunzi kutoka kanda ya Kask...
XERIN AIR CARGO YALETA NDEGE YA MIZIGO TOKA DUBAI
-
*Kampuni ya Xerin Group inajivunia kutangaza kuzindua rasmi huduma yake
maalum ya kuasafirisha Mizigo kwa njia ya Ndege, hatua kubwa katika
kuimarisha...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.