ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 15, 2024

TASAF MKOA WA PWANI KUCHELE YAVIWEZESHA MITAJI YA FEDHA VIKUNDI 1,309

 


NA VICTOR MASANGU,PWANI


Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Pwani imeweka mipango madhubuti ya kuendelea kuhakikisha kwamba inapunguza  kwa kiasi kikubwa  kiwango cha umaskini hapa nchini kwa kuwawezesha wananchi mbali mbali kuweza kupata  mahitaji muhimu na kuboresha maisha ya kaya kwa  mtu mmojammoja.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa Tasaf Rose Kimaro wakati wa kikao maalumu cha mwaka utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanatoa fedha taslimu kwa kila kaya na kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.


 Mratibu huyo alibainisha kwmaba kwa sasa maeneo ya utekelezaji katikampango wao katika Mkoa wa Pwani yamegusa katika halmashauri zote tisa ambapo jumla ya kata zipatazzo 133,vijiji 417,na mitaa 73 hadi kufikia mwezi juni 2024 kaya zilizonufaika na mpango huo zilikuwa 18,403 zimehitimu ambapo kaya 17,761 zinaendelea kunufaika zikiwa ni kaya katika vijiji vipya kwa asilimia 30.

Kadhalika mratibu huyo aliongeza kwamba mpango huo unatekelezwa katika sehemu nne ambazo ni utoaji wa ruzuku za msingi na masharti pamoja na miradi ya muda (PWP) lingine ni kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya (LE).



Kadhalika alisema kuwa wameweza kutekeleza na   kufanya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu,afya, soko (TI) huku nne ikiwa ni utoaji wa mafunzo mbali mbali.

Pia alifafanua kwamba jukumu lingine la Mkoa katika utekelezaji wa mpango huo ni kuhakikisha lengo la serikali la kupunguza kiwango cha umasikini linatimia kama inavyoelekezwa katika ilani ya chama cha mapinduzi ibara ya 25 (n).

  Kadhalika alisema kwamba jukumu lingine ni kendelea  kuboresha kasi ya utekelezaji ya awamu ya tatu ya Tasaf ilikuwafikia wananchi masikini katika vijiji pamoja na mitaa yote                                                                                                                                          
 kwa kutekeleza miradi ya kutoa fursa za ajira za muda, kukuza uchumi wa kaya na kuendeleza rasilimali watu.

Mratibu huyo akizungumzia katika upande wa mafanikio amesema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapatia kiasi cha fedha zaidi ya bilioni  40 ambazo zimeweza kutumika katika kukuza uchumi wa kaya kwa ruzuku za elimu na afya ,ikiwa sambamba na upatikanaji wa chakula na uboreshaji wa miundombinu ya elimu afya, soko pamoja na ujuzi na stadi za maisha.

Pia alisema kwamba jumla ya miradi ya miundombinu ya afya,maji na elimu 13 yenye thamnai ya kiasi cha shilingi bilioni 2.2 imetekelezwa katika ngazi za Wilaya ambapo jumla ya miradi  6 tayari imeshaanza kutoa huduma pamoja na ajira za muda (PWP) zipatazo 647 yenyethamani ya shilingi bilioni 4.5.

Katika hatua nyingine alibainisha kamba hadi kufikia juni 2024 jumla ya wanufaika wapatao 15,740 sawa na kiwango cha asilimia 50 ya wanufaika 31,697 wameweza kujiunga na mfumo wa upokeaji wa ruzuku kwa njia ya mtandao (Simu banki) ambapo pia wanafunzi 96 wameweza kujiunga na vyuo vikuu wakiwemo wasichana 50 pamoja na wavulana 46.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ameupongeza mfuko huo wa Tasaf kwa kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kuzifikia kaya mbali mbali na kuweza kuzisaidia katika nyanja mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.