ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 8, 2013

MAANDALIZI YA PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 YAENDELEA KWA KASI NZURI.





Na Fabian Fanuel
Mratibu wa Pasaka Gospel Festival Albert George Sengo akiongea na Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu waimbaji waliokubali kuimba katika Tamasha la Pasaka Gospel Festival 2013 litakalokuwa sambamba na Uzinduzi wa Studio za Digitali Za Cosu Universal Studio jijini Mwanza.

Waimbaji kumi kutoka Dar es salaam, Mbeya, Iringa, Arusha wanatarajia kutumbuiza katika jumuiko la Pasaka Gospel Festival 2013 litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 31/3/2013 jumapili ya pasaka na tarehe 1/4/2013 katika uwanja wa CCM Katoro jumatatu ya pasaka Geita kuanzia saa nane kamili mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa tamasha hilo bwana Albert George Sengo amesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri sana na kuwaomba wakazi wa jiji na Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Jirani kujitokeza kubarikiwa na waimbaji hawa wa nyimbo za injili.

Amewataja waimbaji hao kuwa kutoka Dar es salaam ni Enock Jonas maarufu kama Zunguka Zunguka, Neema Mwaipopo maarufu kama Raha Jipe Mwenyewe, Nesta Sanga, Daniel Safari, John Shaban, Jessica Julius na Isaya Msangi. Kutoka Mbeya Tumaini Mbembela, Kutoka Iringa Dan Sanga, Kutoka Arusha Neema Munis. 


Sambamba na waimbaji hao wapo waimbaji kutoka jiji la Mwanza kama vile Cecilia Kassim, Goodluck Gozbert, Vijana kwaya Nyamanoro, Eagt City Centre na kwaya nyingine ziadi ya ishirini kutoka Mwanza na nje ya Mwanza.


Amekitaja kiingilio katika tamasha hilo la Pasaka Gospel Festival 2013  ni 2000/= kwa kila mtu, Mwanza na Geita na pia siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa studio mpya ya audio na video ya Cosu Universal Studio iliyoko jijini Mwanza.

Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na taasisi wamekubali kuhudhuria tamasha hilo kubwa la Pasaka Gospel Festival 2013 ambalo halijawahi kutokea jijini Mwanza. 
p

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.