Shughuli ya usanifu ikiendelea chumba cha madaktari wa video. |
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakipata maelezo toka kwenye chumba cha mtayarishaji wa Muziki wa kampuni ya COSU Entertainment jijini Mwanza. |
Hapa kazi iliyokuwa ikisubiriwa ni Sheilah Sezy wa Gazeti lililokuja na mabadiliko makubwa sokoni hivi sasa la Mwananchi kukaanga chips aka kupiga drums. |
Ndipo chips zikakaangika... |
Hili ndilo gari la PA (matangazo ya barabarani) la Great Zone iliyo ndani ya COSU Entertainment. |
Mjengo wa COSU Entertainment ulioko Nyegezi jijii Mwanza. |
UZINDUZI WA KAMPUNI
ILIYONUIA KULETA MAPINDUZI KWENYE SOKO LA DIGITALI MWANZA COSU ENTERTAINMENT
UTAKAOFANYIKA TAREHE 31/03/2013 SIKU YA PASAKA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA .
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Ndugu zangu
wanahabari.
Ujio wa COSU Intertainment unakuja wakati Tanzania
ikishuhudia Media zake zikiingia katika mfumo wa digitali ambao unahitaji
kulishwa ipaswavyo ili kuvutia wadau na wafanyabishara kuweza kushawishika
kununua muda wa vipindi husika (kuwa wadhamini) jambo ambalo huchangia kwa
kiasi kikubwa maendeleo ya utoaji huduma kwa media mbalimbali hapa nchini.
Ikumbukwe
kuwa awali Taifa letu lilikuwa kwenye mfumo wa Analojia ambao ilikuwa ukiwa na
Luninga yako na nishati na antenna yako ya waya basi mawasiliano utayapata
utatizama Tv yoyote hata vipindi visivyokuwa na ubora au usivyokuwa na mpango navyo alimuradi tu
umetizama TV, sasa hizo zama zinatoweka taratibu mikoa baada ya mikoa.
Walianza
Dar es salaam, Dodoma, Tanga sasa Mwanza nayo imeingia kwenye mfumo wa digitali
mwisho wa siku wilayani, vijijini na Taifa kwa ujumla litakuwa digitali.
Kwa hali ya
sasa ndani ya mfumo wa digitali ili upate mawasiliano ya televisheni lazima uwe
na king’amuzi ambacho unalipia, sasa wamiliki wa ving’amuzi tulivyonavyo (vi 3
sasa) ili kuvutia wateja kwa malengo ya kupata soko kubwa wanalazimika kuweka
channel zenye mvuto na zenye ubora ili kukidhi soko la ushindani.
Kupitia
ushindani itafika kipindi ndani ya king’amuzi kimoja kutakuwa na chanel 200 hivi za ndani na nje hapa tutashuhudia tukishindanishwa
na televisheni za kimataifa, kwa mfumo huu vituo vingi vitakuwa vikishindana
kwa kuwa na maudhui nzuri na kuwa na vipindi vya kipekee ili vipate matangazo na wadhamini wa kutosha.
Ni suala
lililo wazi kuwa wenye matangazo yao hukimbilia vituo vinavyotizamwa.
Media kwa
sasa ziko kwenye mahitaji ya kiushindani, hivyo zina mahitaji na mahitaji, kwa
mtindo huu basi COSU Entertainment tumeona kuwa kuna mwanya hapo, nasi ni vijana
wakongwe katika tasnia ya media tuko kwaajili ya kuuziba mwanya huo, na hizi
ndizo juhudi sasa za kuitikia wito wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA
kuzifanyia kazi zile ajira ambazo tumeelekezwa zipo nasi kushuhudia kweli zipo.
COSU
Entertainmen tuliojikita zaidi katika uandaaji na utayarishaji kuanzia vipindi,
Audio music, Video za muziki pamoja na kujenga jukwaa la vipaji mbalimbali nchini
Tanzania tumeliona soko hilo la ajira na sasa tunataka kuudhihirishia umma wa
Watanzania kuwa mapinduzi yatafanyika kupitia sisi.
Hatujaishaia
hapo pia tumeliona soko jingine la ajira lililopo vijijini na wilayani hapa
tunazungumzia Muziki wa Asili, huu ni muziki ambao kwa sasa vionjo vyake
vinakuja kwa kasi na kuboresha muziki wa kisasa na muziki huo wa asili
ukionyesha kuwa na dira ya maisha marefu sokoni.
Tizama
marafiki zetu Afrika Magharibi, Afrika ya kati, Afrika ya kusini wote hao
vionjo vya muziki asili vimechangia kuubeba sana muziki wao kutamba katika soko
la kimataifa na sasa ndiyo wameiteka dunia.
Mifano iko
mingi – akina Werason, Koffi Olomide,
Fally Ipupa, J. Martins na wengine wengi wote hawa style zote mpya wanazokuja nazo
nyingi zinatoka vijijini, ambako hufanya mashindano ya vipaji mbalimbali iwe
waimbaji, wapigaji muziki hadi wachezaji na kuubebea muziki huo kwenye soko
hatimaye makubwa mapinduzi tunayashuhudia.
Sasa kwa
hili tukirejea nchini na kuanzia hapa Kanda ya ziwa, Kanda inayosifika sana kwa
vipaji vya nyimbo asili tena za kuchezeka, anzia Kagera kwa akina Saida Karoli,
Maua, Papaa Kishaju wote muziki wao unadumu, Ingia Shinyanga kuna ngoma asili
pale kama Bolaboka, Wigashe, Bogobogobo, rudi Mwanza na wilaya zake nenda
Ukerewe na Kadogoli, Dungu, ngoma nyingi za kuchezeka tena za kusisimua na hata
tumeshuhudia mara nyingine zikitumika kwenye maharusi na dhifa mbalimbali na kadhalika.
Hivyo basi
nina uhakika tukitumia vyema muziki huu mengi yatafanyika.
Katika
project tutakazozifanya kuna watu wakajkuja kwetu kurekodi kwa fedha na kuna
watu tutawasaka nao warekodi kwa gharama zetu hawa ote tutashirikiana nao
kutengeneza matirio zenye maudhui ya kuuzika, zenye Ushawishi.
Ndugu zangu
waandishi wa habari huduma zetu ingawa zimeanza kufanya kazi kwa kurekodi
baadhi ya vipindi kwaajili ya vituo vya televisheni mbalimbali, pamoja na
kurekodi video za kwaya na bendi mbalimbali kwa sasa, uzinduzi rasmi tutaufanya
mnamo tarehe 31/03/2013 katika sherehe ya sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM
Kirumba ambapo tutatoa burudani ya Muziki wa Injili tuliyoipa jina la PASAKA
GOSPEL FESTIVAL ambapo wakazi wa Mwanza watashuhudia burudani ililoandaliwa kwa
ubunifu wa hali ya juu ikishirikisha waimbaji wakubwa kama Enock Jonas
(ZUNGUKA), na Neema Mwaipopo (RAHA JIPE MWENYEWE).
Wengine ni
Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi
(SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa
na Neema Munisi.
Kwaya za
mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre
kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Uzinduzi Pasaka hii.
Jumatatu ya
pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro
Kiingilio
kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu
Hivyo
tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.
Nanyi ndugu
zangu wanahabari twawaomba mtusambazie habari hizi kwani hili linatoka kwa watu
wenu na msishangae waandishi nanyi kupitia vipaji vyenu mkapata fursa katika soko la
ajira la COSU Entertainment, tukawa tukiwakodisha mara kadhaa kutokana na
either kuzidiwa na mahitaji hivyo tunawasihi msisite kufungua milango ya
ushirikiano ili tujenge Tanzania yetu.
Zidumu fikra
za Maendeleo!
Aksanteni
kwa kutusikiliza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.