ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 5, 2013

KANUSHO JUU YA MTU ANAYEJITAMBULISHA KWA JINA LA “BUKOBA WADAU” KWENYE MTANDAO WA JAMIIFORUMS


Tunapenda kuutaarifu umma kuwa BUKOBAWADAU MEDIA, wamiliki wa Blog ya http://bukobawadau.blogspot.com/ na waendeshaji wa Wadau Club kwenye mtandao wa Facebook inayopatikana https://www.facebook.com/groups/171636729552100/ hatuna uhusiano wowote wala maslahi na mtu anayejiita Bukoba Wadau kwenye mtandao wa Jamiiforums ambaye wasifu wake unapatikana hapa http://www.jamiiforums.com/member.php?u=122775.

BukobaWadau kama chombo cha habari tunazingatia miiko yote ya utafutaji na usambazaji wa habari ikiwemo uhuru wa kutofungamana na upande wowote katika kutoa habari. Ni masikitiko yetu kwamba habari na taarifa zinazoegemea upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na mtu anayetumia jina letu, zinatuweka katika uchonganishi kati yetu na wadau na wale wote wanaoathirika na mchezo wa matumizi mabaya ya jina letu kwenye mtandao wa Jamiiforums.

Katika kukabiliana na mchezo huu, tumeanza kwa kuwasiliana na wenzetu wa Jamiiforums tukiwaomba msaada wa kumdhibiti mhusika. Tunaamini watatupa ushirikiano wa kutosha kulimaliza tatizo hili kwa suluhisho la kudumu. Lakini pia ikumbukwe Bukoba Wadau pamoja na nembo yake ambavyo vyote vinatumiwa na mhusika ni mali halali za ubunifu za BUKOBAWADAU MEDIA. Zipo kisheria na zinalindwa na sheria za hati miliki. Kwa kuwa mchezo wake ni mauti ya chombo na Biashara yetu, iwapo ataendelea na udurufu wa mchezo huu, basi tutaanza kwa kuanika wazi mhusika kwa majina halisi na wasifu ili jamii imtambue kabla ya kumchukulia hatua za Kisheria.

Mwisho tunapenda kuwashukuru Wadau wetu wote kwa jinsi ambavyo mmeendelea kutuunga mkono kwa namna moja au nyingine. Nasi tunawaahidi kuendeleza huduma bora katika kuwaletea taarifa za matukio na habari za ukweli na uhakika zisizoegemea upande wowote.

Imetolewa na Uongozi wa BUKOBAWADAU MEDIA

Best Regards,

Mc Baraka 
Manager (Founder)
BUKOBAWADAU
P.O.BOX 316
Bukoba

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.