Wafuasi wa Hugo Chavez wamekuwa wakimuombea aweze kuugua pole |
Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini
Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza kupokea matibau. Hata hivyo
maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika
mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa
kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Ujumbe wa JeshiBwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa tangumaradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.
Taarifa kutoka kwa jeshi
imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia
jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na
wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.
Chavez - wasifu
Hugo Chavez alijitosa katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa
luteni katika jeshi. Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos
Andres Perez.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini
baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo. Katika
kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango
yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake
na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika
muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba,
ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya
wapiga kura.
Rais Chavez
alitaifisha rasilmali ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi
zilimfanya azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji
mkono mkubwa wa watu maskini.
Chavez na jamii ya
kimtaifa
Kutokana na urafiki
wake na viongozi wa mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro,
ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani,
ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.
Chavez alipendwa
nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na
katika nchi za nje. Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia
kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni
alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua
uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.
Hisani ya BBC SWAHILI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.