Usiku wa kuamkia October 25 mwaka 2021, ulikuwa mgumu kwa Mkurugenzi wa moja ya viunga vya burudani vyenye hadhi ya kitalii jijini Mwanza kwani Kiwanja Maarufu Mwanza, The Cask Bar & Grill kiliteketea kwa moto na kuacha maswali mengi ya utata kwamba huenda ingekuwa ndiyo mwisho wake.
Meneja wa KCB Bank tawi la Mwanza, Emmanuel Greyson Mzava, anasimulia alivyolishuhudia tukio hilo na namna benki hiyo ilivyoshiriki harakati za kuirudisha hadhi ya eneo hilo ambalo licha ya kutumika kama sehemu ya burudani pia ni moja ya maeneo yanayo kuza uchumi wa 'Jiji la Sato na Sangara' sanjari na kuisaidia Serikali katika ubunifu wa kuzalisha ajira hasa kwa vijana.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.