Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali
Na Oscar Assenga,TANGA
Kituo cha Sayansi cha Stemp Park kilichopo Jijini Tanga kimeleta Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya elimu ambapo kimeweza kuwa kichocheo kwa Wanafunzi kuhamasika kupenda kusoma Masomo ya Sayansi na kuongeza ubunifu.
Stemp Park ipo katika kata ya Kisosora na imeleta mapinduzi makubwa katika masomo ya Sayansi kwa Wanafunzi pamoja na Walimu.
Wanafunzi wanaotumia kituo hicho katika mambo ya Sayansi ni kianzia Chekechea hadi shule za Sekondari.
Akizungumza juzi katika wiki ya Sayansi Afrika Meneja wa kituo hicho Maxi George wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa Kwake iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya sayansi katika bara la Afrika
Ambapo alisema idadi kubwa ya ubunifu wa kisayansi katika jiji la Tanga umekuwa mkubwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakienda kituo hicho na kufanya shughuli zao za ubunifu ambapo wanafanya wa nadharia zaidi.
"Hapa vijana wanapata nafasi ya kuelezwa umuhimu wa Sayansi katika maisha ya kawaida,na katika maisha ya shule kwa kujifinza mambo mbalimbali ya sayansi kwa vitendo na kwa kuona"alisema George
Katika hatua nyingine kituo hicho pia kinawanufaisha walimu wa mkoa wa Tanga kwa kuwapa ujuzi katika kuwafundisha wanafunzi shuleni
"Walimu wanaprogram maalum ambayo inaitwa TOT hii imekuwa chachu ya kuwapa ujuzi katika kuwafundisha vijana,lengo likiwa ni kuchagiza ufaulu kwa masomo ya sayansi"alisema George
Pia aliwaasa wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wajifunze masomo ya Sayansi kuwa sio ngumu bali watu waliaminiashwa kuwa ni ngumu
"Tunatoa wito kwa Wazazi,kuwaachia watoto wajifunze zaidi,pale mtoto anapofanya jambo la ubunifu mzazi amwache akifanye ili apate njia sahihi ya kutengeneza kitu anachokitaka ambacho badae kinaweza kuwa na manufaa"alisema George
Aidha Wanafunzi wanaoenda kwenda kujifunza katika kituo hicho wameeleza kuwa kituo hicho kimewajenga zaidi kwa kuwa wabinifu.
Mmoja wa wanafunzi wa kike Rukia Omari wa Masechu Sekondari anayenda kupata elimu ya Sayansi katika kituo hicho alisema wao wanakabiliwa na changamoto pindi wanapotaka nafasi ya kwenda kujifunza katika kituo hicho kwa kuwa wazazi wanawabana kupatamuda wa ziada ya kujifunza Sayansi
"Mazingira tunayoishi inatufanya wasichana tusiwesawa na wavulana katika kujifunza,ukiomba ruhusa kwenda kujifunza huwezi kupewa,utaambiwa bora umsaidie Mama kazi hivyo kufanya mua wa kusoma usiwepo lakini kwa wanaume iko tofauti akirudi hana kazi"alisema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.