Mahakama ya watoto itahusika katika mambo yote yanayohusu
watoto. Ikiwa mtoto amefanyiwa vitendo vilivyotajwa hapo juu,
wazazi/mwanajamii anaweza kutoa taarifa katika serikali ya mtaa,
ambayo kwa kushirikiana na afi sa ustawi wa jamii, wana wajibu wa
kufuatilia ulinzi na ustawi wa mtoto huyo aliyedhurika.
Ikihitajika
kwenda mahakamani, afi sa ustawi ana wajibu wa kupeleka maombi
mahakamani juu ya nafuu ya au ulinzi wa mtoto huyo.
Angalizo: Serikali ya mtaa ina wajibu kutokana na sheria ya mtoto,
kuwatafutia na kuwapa hifadhi watoto ambao wametelekezwa au
kukosa makazi.
Pia ina wajibu, kwa kushirikiana na afi sa ustawi wa
jamii, kuwatafuta wazazi waliotelekeza watoto na kuwarudisha, au
kutoa amri ya matunzo.
Shirika la Kutetea Haki za Watoto wafanyakazi Nyumbani la Nuru Organisation.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.