ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 31, 2022

COASTAL UNION WATIMIZA AHADI YA RC ADAM MALIMA

 

Wachezaji wa Coastal Union wakiwania mpira dhidi ya wa Azam FC wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA iliyopigwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Sheirh Amri Abeid Jijini Arusha ambapo Coastal Union ilishinda


NA OSCAR ASSENGA,ARUSHA

MATOKEO ya UshindI walioupata kwa Penalti 6 kwa 5 hadi kuitoa Azam FC kwenye tumaini la kucheza Fainali za Kombe la Shirikisho ni kama sehemu ya Kikosi cha Coastal Union ya Tanga wametimiza Ahadiwaliyoitoa kwa Mkuu wao wa Mkoa Adam Malima.
 

Kabla ya mchezo huo wa nusu fainali za FA kati ya Coastal dhidi ya Azam, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alitembelea Kambi yA Wagosi wa Kaya huko Mbauda Jijini Arusha.

Katika mazungumzo yake na wachezaji Malima aliwaeleza kuwa wana kila sababu ya kuifunga Azam kwa madai kuwa wameshawahi kucheza nao huku wakiweza kuonyesha kiwango kikubwa mchezoni.

Mbali na hayo Malima alisema, Kikosi hicho cha Coastal kitakapoibuka kidedea kwenye mchezo huo kitaleta sifa njema kwa Mkoa huku akitumiafursa hiyo kuwapatia wachezaji donge nono.

"Najua nina deni lenu niliahidi na nitawapa hata hivyo mchezo huu mnapaswa kushinda na nitawapa kiasi kingine cha fedha"alisikika RC Malima akiwapa morari wachezaji wa Coastal.

Baada ya kusema hayo, nahodha wa Coastal Amani Kyata alimhakikishia Mkuu wa Mkoa Adam Malima kwamba wataishinda Azam kwenye mchezo huo.

Coastal imeifunga Azam kwa Penalti 8 kwa 5 ambapo sasa timu hiyo yenye maskani yake barabara 11 Jijini Tanga itacheza Fainali na Dar Young African.


NGOMA ya Baikoko imeonekana kuwa Nyenzo waliyoitumia Mashabiki wa Coastal katika kuwapa nguvu Wachezaji wao na hivyo kukiwezesha Kikosi cha Wagosi wa Kaya kutinga Fainali za Kombe la FA.


Kabla ya mchezo wa nusu fainali kupigwa, majira ya asubuhi mashabiki wa Coastal waliteka Viunga vya Jiji la Arusha kwa kupiga na kucheza ngoma yao ya Baikoko.

Kitendo hicho cha kuzunguka wakitumbuiza kwa ngoma hiyo mitaani huku  wakionyesha vidole vitatu kama ishara ya ushindi hatua ambayo ilionekana kuleta furaha kwa wapenzi wengi wa soka.

Pamoja na kuzunguka mitaani kwa shangwe, mashabiki hao walihamia mtaa
wa Mbauda walikofikia Coastal na kulakiwa na wachezaji ambao nao
walionekana kuwa na ari ya ushindi.

Shangwe na nderemo zilihamia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mashabiki
kupiga ngoma ya Baikoko wakiishangilia timu yao wakati ikicheza hadi
ilipoibuka mshindi.

Mchezo ulikuwa wa vuta nikuvute kwa timu zote kushindwa kupata mabao
hadi dk 90 zilipomalizika na kuongezwa dk 30 nazo zikamalizika kwa
sare hadi ilipofika hatua ya Mikwaju ya Penalti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.