ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 10, 2010

KITABU CHA JK CHAZINDULIWA IKULU.

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Wasifu wa Maisha yake, akishuhudiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Julius Nyang'oro jana mchana Ikulu, Dar es salaam

Mwandishi wa Kitabu cha Wasifu wa JK Profesa Julius Nyang'oro akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kitabu hicho ambacho alikiandika na kuelezea sababu mojawapo iliyomfanya aandike kitabu hicho ni kutokuwa na kitabu cha aina hiyo kwa viongozi wetu wa nchi isipokuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakiongea na Profesa Nyang'oro ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Wasifu wa JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na Bi. Amina Mtengeti ambaye ni Shangazi wa Profesa Nyang'oro mwandishi wa kitabu cha JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Pichani ni viongozi wengine wa kitaifa na marafiki wa Profesa Nyang'oro waliohudhuria uzinduzi huo.

Vitabu hivyo vimeanza kuuzwa kwenye duka la vitabu la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam rasmi kuanzia leo tarehe 10-12-2010 kwa gharama ya shillingi 25,000/=


PICHA KWA HISANI YA IKULU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.