Waziri Nchimbi akifungua mkutano huo kwa ishara ya kukata utepe.
Waziri Nchimbi akitambulisha Cheti cha Ufunguzi. "Nitafarijika sana Ikiwa wasomi wengi watajihusisha na kuwekeza katika kilimo cha kisasa na ufugaji" Sehemu ya hotuba.
Mkutano huu ni matokeo ya maazimio ya mkutano uliofanyika Dodoma Mwezi juni ambapo uliazimia kufanyika kwa mikutano kama hii ya vijana katika kila kanda ili kujadili changamoto mbalimbali za kimaendeleo.
MA-FOUNDER WA TAYODEFO Kutoka kushoto ni Emmanuel Mgenge, Mgunda Bwere, Patrick Bryoba, Tumaini Kimaro na Christina Benard.
Wataalam wa maendeleo wanaamini kuwa elimu na fedha ni rasilimali muhimu kwa maendeleo hivyo mkutano uliopita wa Dodoma uliazimia pia Uanzishaji wa Benki ya Vijana.
Waziri nchimbi akiagana na wanavyuo mara baada ya kumwakilisha waziri mkuu (Mizengo Pinda) kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa vijana vyuo vya elimu ya juu uliofanyika katika ukumbi wa BOT CAPRIPOINT, MWANZA.
Kutoka kushoto: Mdau wa TAYODEFO, Mh.NCHIMBI na G.SENGO.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na Ma-FOUNDER wa TAYODEFO. Vyuo vilivyoshiriki ni pamoja na Chuo kikuu cha mtakatifu Agustin (SAUTI), Chuo kikuu kishiriki cha Afya Bugando (BUCHS) na Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Mwanza. Mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya vijana kupigana vita juu ya UKIMWI na Madawa ya kulevya nayo ndani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.